Nenda kwa yaliyomo

Mlamani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kulungu mwekundu na ndama wawili wakila majani
Kiwavi anakula

Walamani (kwa Kiingereza: herbivores) ni wanyama wanaokula mimea pekee au hasa[1]. Maumbile yao yanalingana na chakula cha kimea na yanahusu hasa mdomo au viungo vya kukatakata chakula halafu matumbo yaani viungo vya kumeng’enya chakula. Viungo hivi ni tofauti baina ya walamani na walanyama.

Walamani wanashirikiana mara nyingi na bakteria maalumu wanaoishi katika matumbo na kuzalisha vimeng'enya vinavyowawezesha kuvunja kwa mfano selulosi ya mimea[2].

Spishi nyingi za walamani hula hasa aina fulani za mimea. Mfano ni panda mkubwa anayekubali majani ya mwanzi pekee.

Kuna walamani wanaokula wakati mwingine pia protini, kwa mfano mayai. Mlanyasi kama ng'ombe hula pia wadudu waliopo kwenye nyasi.

Wanyama wanaoweza kula nyama pamoja na majani wakifanya hivyo mara kwa mara hawahesabiwi kati ya walamani bali huitwa walavyote.

Kuwepo kwa walamani ni msingi kwa kuwepo kwa walanyama. Kiekolojia walamani hutumia nishati iliyokusanywa ndani ya mimea kwa njia ya usanisinuru halafu wanawindwa na walanyama.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Herbivore, tovuti ya sciencedaily.com
  2. Symbiosis, tovuti ya cell.com
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mlamani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.