Justin mfiadini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya Kirusi ya Mt. Justin.

Justin (pia Yustino Shahidi; Kiing. Justin Martyr; alizaliwa Flavia Neapolis, leo Nablus, Palestina, 103 hivi - Roma, Italia, kati ya 162 na 168) alikuwa mwanafalsafa ambaye, kisha kuongoka, alieneza na kutetea Ukristo hata kwa maandishi maarufu, na hatimaye akauawa pamoja na wanafunzi wake sita (Karitoni, Karito na wenzao Evelpisto, Gerasi, Peoni na Liberiani) katika dhuluma ya Dola la Roma.

Hati za mateso yao zimetunzwa hadi leo[1].

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Walutheri na Waanglikana kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Juni[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Maandishi yake[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Acta S. Iustini et sociorum
  2. Martyrologium Romanum

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Iustini opera, 1636

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.