Nenda kwa yaliyomo

Jeshi la Wanamaji la Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Naval bendera

Jeshi la Wanamaji la Kenya ni tawi la Majeshi ya Ulinzi ya Kenya upande wa baharini. Makao makuu yako katika mji wa Mombasa.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Jeshi la Wanamaji la Kenya lilianzishwa tarehe 12 Disemba 1964, mwaka mmoja baada ya Kenya kupata uhuru.

Lilitanguliwa na Nevi ya Kifalme ya Afrika ya Mashariki (REAN).[1]

Baada ya REAN kuvunjwa mwaka 1962, Shirika la Reli na Bandari la Afrika ya Mashariki lilichukua mamlaka ya udhibiti wa shughuli za majini katika maeneo yaliyokuwa makoloni ya Afrika Mashariki hadi nchi huru zikaunda nevi zao.

Meja JCJ Kimaro alikuwa Kamanda wa kwanza wa Jeshi la Wanamaji la Kenya. Aliteuliwa na Jomo Kenyatta.

Tarehe 4 Septemba 2012 Nevi ya Kenya ilishiriki kuvamia jiji la Kismayo katika juhudi za pamoja za Umoja wa Afrika kulikomboa kutoka wanamgambo wa Al-Shabaab katika Vita vya Somalia.[2]

Majina ya vyeo katika Nevi ya Kenya ni kama ya vikosi vya ardhi:

Vyeo vya maafisa kuanzia chini

  1. "Kenya Navy: History". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-02-19. Iliwekwa mnamo 2018-03-17.
  2. "Kenya's navy shells Kismayo in Somalia", BBC, 4 September 2012. Retrieved on 4 September 2012.