Nenda kwa yaliyomo

Jiometri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Jeometri)
Jiometria inajulisha ukubwa wa pembetatu.

Jiometri (pia: Jiometria, kutoka neno la Kigiriki γεωμετρία, geometria, linaloundwa na geo- "dunia" na -metron "kipimo", kwa kupitia Kiingereza geometry) ni tawi la hisabati linalochunguza ukubwa, mjao, umbo na mahali pa eneo au gimba.

Tawi la jiometri linalochunguza pembetatu hasa huitwa trigonometria.

Maumbo huwa na nyanda (dimensioni) mbili yakiwa bapa, au tatu kama ni gimba. Kwa mfano mraba, pembetatu na duara ni bapa na kuwa na nyanda 2 za upana na urefu. Kumbe tufe (kama mpira) au mchemraba huwa na nyanda 3 za upana, urefu na kimo (urefu kwenda juu).

Jiometri za kitambo

[hariri | hariri chanzo]

Maumbo ya jiometri yalionekana kwanza nchini Mesopotamia na Misri katika milenia ya pili baada ya Yesu Kristo. Maumbo haya yalikuwa na urefu, uwanda ambazo zilitumika katika kupima ardhi na kuzuru sayari nyingine.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Jiometri hutumiwa kupima eneo na mzingo wa umbo bapa. Inaweza kupima pia mjao na eneo la uso wa gimba.

Katika maisha ya kila siku jiometri inasaidia kujua vipimo vya vitu vingi kama vile:

  • eneo wa uso wa chumba na hivyo kuamua kiasi cha rangi kinachohitajika kwa kupaka rangi kuta zote.
  • Mjao wa chombo ili kujua kuna lita ngapi za maji ndani yake.
  • Eneo la shamba linalotakiwa kugawiwa kati ya watu.
  • Urefu wa mzingo wa bwawa ili kujua tunahitaji kununua mita ngapi za fensi tukitaka kuifunga.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Chanzo cha jiometri kilikuwa elimu ya kupima ukubwa wa eneo fulani, kwa mfano eneo la mashamba ya kijiji kwa kusudi la kuligawa kati ya watu wake.

Mtaalamu wa Ugiriki ya Kale aliyeitwa Euklides alitunga kitabu cha kwanza kinachofahamika kuhusu jiometri.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jiometri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.