Euklides

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Euklides (takr. 365 KK - 300 KK, Kigiriki Εὐκλείδης Eukleidēs, Kiing. Euclid) alikuwa mwanahisabati wa Misri ya Kale. Aliitwa pia Euklides wa Aleksandria akihesabiwa pia kati ya wataalamu wa Ugiriki ya Kale.

Anaitwa mara nyingi "Baba wa Jiometria". Habari zake hazina uhakika kamili kuhusu miaka ya maisha yake lakini anaaminiwa alitokea katika familia ya Kigiriki akaishi huko Aleksandria wa Misri wakati wa farao Ptolemaio I (323 KK–283 KK).

Hakuna mengi yanayojulikana kwa hakika juu ya maisha yake. Huaminiwa ya kwamba alizaliwa Aleksandria mnamo 365 KK alapata mafunzo ya juu kwenye akademia ya Athens. Kazi yake alifanya wakati wa Farao Ptolemaio I alifundisha hisabati.

Alikuwa maarufu kwa njia ya vitabu vyake 13 vinavyofundisha hisabati vilivyoitwa Στοιχεῖα stoicheia au "Misingi". Tafsiri za vitabu hivi zilitumiwa hadi karne ya 19.