Hospitali ya Dareda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hospitali ya Dareda ipo mkoani Manyara, ambapo ilianzishwa mwaka 1948, ipo eneo Kanisa Katoliki la Dareda. Muda wa saa za kazi ni kuanzia 8:00 asubuhi mpaka 5:00 jioni, Jumatatu mpaka Ijumaa na kwa siku za Jumamosi na Jumapili huduma zinaanza saa 12:00 mchana. Pia wanatoa huduma nyingine ambapo wana Shule ya Unesi inayoitwa Dareda School of Nursing. [1]

Huduma zinazotolewa ni: Wodi za kulaza wagonjwa, huduma ya wagonjwa wa nje wasiolazwa, famasi, mazoezi ya viungo, Maabara, X-RAY/Mionzi, Chumba cha Upasuaji, Ofisi za utawala, Shule ya Unesi na Mgahawa wa chakula [2]

Hospitali hii inaendeshwa na Jimbo Kuu Katoliki la Mbulu na inakadiriwa kuhudumia karibia watu 130 kwa siku na ina idadi ya vitanda 200. Hospitali ina uongozi bora ulio makini na walio na uangalizi mzuri ambapo wanadumisha weledi na mahusiano mazuri kati yao wenyewe na kuna wanathamini kuheshimiana kiukweli ambapo inasaidia kuongoza vizuri huduma ya hospitali na thamani ya huduma inayotolewa.

Kwa wagonjwa wanaolazwa kuna wodi nne (4)ambazo ni: wodi ya watoto chini ya miaka 12, wodi ya wanaume, wodi ya wanawake na wodi ya Mama na Mtoto. Kila wodi ni kubwa na pana yenye vitanda. Hospitali ya Dareda ingekua na Mapazia ingekua Hospitali yenye hadhi ya daraja la juu (luxury) [3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]