Fatma Karume

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Fatma Karume (amezaliwa tarehe) ni mwanasheria, wakili wa kujitegemea, mwanaharakati ambaye aliwahi kuwa rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019. Alipata wadhifa huo baada ya kushinda katika uchaguzi wa urais wa chama hicho uliofanyika Aprili 2018 na hivyo kumrithi mtangulizi wake Tundu Lissu aliyekiongoza chama hicho kutoka mwaka 2017 hadi 2018.[1][2][3] Katiba ya chama cha TLS hurusu kuongoza kwa muda wa mwaka mmoja tu. Rugemeleza Nshala alichaguliwa katika uchaguzi huo kuwa Makamu wa Rais wa chama hicho.[4]

Alikuwa rais wa TLS hadi mwaka 2019 Dr. Rugemeleza Nshala alipochaguliwa kuwa rais mpya[5]

Maisha Yake[hariri | hariri chanzo]

Fatma Karume ni mtoto wa rais mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume[6].

Anaongea kwa ufasaha lugha tatu ambazo ni: Kiswahili, Kiingereza na Kifaransa[7].

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Fatma Karume ni mwenza katika kampuni ya mawakili ya IMMMA yenye makao makuu katika jiji la Dar es Salaam - Tanzania[9].

Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 25 katika nyanja ya sheria. Alisajiliwa kama wakili kwa Tanzania na Zanzibar mwaka 1994[10]. Ni mbobezi katika sheria za kodi na ameshawahi kuwakilisha benki kubwa katika kesi mbalimbali.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fatma Karume kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.