Nenda kwa yaliyomo

Frederik Willem de Klerk

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka FW de Klerk)
Frederik Willem de Klerk
Frederik Willem de Klerk 1990.jpg
Frederik Willem de Klerk 1990.jpg
makamo wa rais
Tarehe ya kuzaliwa 18 Machi 1936
Tarehe ya kifo 11 Novemba 2021
Alingia ofisini 1994 hadi 1996
Aliondoka ofisini 1997
Kazi Rais


Medali ya Tuzo ya Nobeli
Medali ya Tuzo ya Nobeli

Frederik Willem de Klerk (18 Machi 193611 Novemba 2021) alikuwa mwanasiasa wa nchini Afrika Kusini aliyekuwa rais wa nchi.

Maisha

Alizaliwa katika familia ya Makaburu na lugha mama yake ni Kiafrikaans.

Alisoma sheria akawa wakili.

Mwaka 1972 alichaguliwa mbunge kwa chama cha National Party. Mwaka 1976 aliteuliwa kuwa waziri wa ustawi wa jamii akaendelea kuongoza wizara mbalimbali hadi mwaka 1989.

Baada ya rais PW Botha kujiuzulu katika uongozi wa chama cha National de Klerk alimfuata kama mwenyekiti wa chama na kuanzia 20 Sepzemba ya mwaka ule pia kama rais wa nchi.

Alikuwa rais wa Afrika Kusini wa mwisho chini ya mfumo wa apartheid kuanzia 1989 hadi 1994. Alitambua ya kwamba mfumo wa ubaguzi wa rangi umefikia mwisho wake akaanzisha majadiliano na wanasiasa wa ANC akaamuru kumwachisha Nelson Mandela kutoka gerezani akaandaa pamoja naye mabadiliko ya mfumo wa kisiasa yaliyoleta uchaguzi huru wa kwanza nchini ambapo raia wote waliweza kushiriki.

Mwaka 1993 alipokea Tuzo ya Nobel ya Amani pamoja na Nelson Mandela.

Kuanzia 1994 hadi 1996 De Klerk alikuwa makamu wa rais Nelson Mandela.

Mwaka 1997 akastaafu na kuachana na shughuli za siasa.

Alioa mara mbli akawa na watoto watatu kutoka ndoa yake ya kwanza.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Frederik Willem de Klerk kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.