Christiane Amanpour

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Christiane Amanpour kwenye Tuzo ya Luncheon Waldorf ya Mwaka 67 ya Mwaka wa Peabody = Hoteli ya Astoria New York, NY USA Juni 16, 2008

Christiane Amanpour Maria Heideh (amezaliwa 12 Januari 1958) ni mwanahabari kutoka nchi za Uingereza na Iran. Amanpour ni mtangazaji mkuu wa kimataifa wa kituo cha televisheni cha CNN. Kila siku ana kipindi chake "Amanpour" anapohoji wageni.

Maisha ya mapema na elimu[hariri | hariri chanzo]

Amanpour alizaliwa mjini London, England akiwa binti wa mama Mwingereza Patricia Anne Hill na baba Mwajemi Mohammad Taghi Amanpour. [1] Baba yake alitoka Tehran . Amanpour alilelewa Tehran hadi umri wa miaka kumi na moja. [2] [3] Baba yake alikuwa Mwislamu na mama yake alikuwa Mkatoliki. Christiane anaongea tangu utotoni lugha za Kiingereza na Kiajemi na ameolewa na Mmarekani Myahudi.

Alisoma shule ya msingi nchini Iran akaendelea na masomo ya sekondari kule Uingereza.

Mwaka 1979, baada ya mapinduzi ya Kiislamu, familia ilihamia Uingereza.

Christiane alihamia Marekani akasoma uandishi wa habari kwenye Chuo Kikuu cha Rhode Island alipomaliza mwaka 1983. [4]

CNN[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 1983, aliajiriwa na CNN kwenye idara ya habari za kimataifa huko Atlanta, Georgia.

Alitumwa nje mara ya kwanza kuleta habari za Vita kati ya Iran na Irak ambako alipata sifa nyingi. Baadaye alihamishwa Ulaya alipoangalia anguko la ukomunisti katika nchi za Ulaya Mashariki. [5]

1990 alitumwa tena Mashariki ya Kati alipokuwa mtoa ripoti juu ya Vita ya Ghuba ya 1990/91, kazi iliyomfanya kuwa mashuhuri duniani. Aliendelea kuleta ripoti juu ya Vita ya Bosnia na kutoka sehemu nyingine penye vita na magombano. Aliripoti kutoka Sarayevo, Bosnia wakati mji ulifyatuliwa risasi kwa mizinga ya Waserbia akieleza kwa undani mateso ya wakazi wa mji na hapo alikosolewa kwamba namna yake ya kuripoti iliacha msingi wa uanahabari kutosimama upande wowote. Hata hivyo alisifiwa kwa uhodari wake kuvumilia hatari. [6]

Kuanzia 1992 hadi 2010, Amanpour alikuwa mtangazaji mkuu wa kimataifa wa CNN Amanpour aliripoti juu ya machafuko makubwa kutoka sehemu nyingi za ulimwengu, pmoja na Irak, Afghanistan, Palestina, Iran, Israel, Pakistan, Somalia, Rwanda, na Balkani na kutoka Marekani wakati wa Kimbunga Katrina . Ametoa mahojiano ya kipekee na viongozi wa ulimwengu kutoka Mashariki ya Kati hadi Ulaya, Afrika na kwingineko, pamoja na marais wa Irani Mohammad Khatami na Mahmoud Ahmadinejad, pamoja na marais wa Afghanistan, Sudani, na Syria, miongoni mwa wengine. Baada ya Shambulio la 11 Septemba 2001, alikuwa mwandishi wa kwanza wa kimataifa kumhoji Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair, Rais wa Ufaransa, Jacques Chirac, na Rais wa Pakistani Pervez Musharraf. Alifanya mahojiano mengi na viongozi wa kimataifa. [7]

2010 aliondoka katika kampuni ya CCN akahamia kituo cha ABC lakini mwaka 2011 alirudi akiendelea kuwa mtangazaji mkuu wa kimataifa wa CNN.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia 1998 hadi 2018, Amanpour alikuwa ameolewa na Mwamerika James Rubin, waziri msaidizi wakati wa serikali ya rais Clinton. . Mtoto wao, Darius John Rubin, alizaliwa mnamo 2000. Baada ya kuishi London hapo awali, walihamia New York City mnamo 2010. [8] Mwaka 2013 walirudi London.

Ilitangazwa mnamo Julai 2018 kuwa Amanpour na Rubin walikuwa wanaachana. [9]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Christiane Amanpour's Biography", ABC News. Retrieved on 23 August 2010. 
  2. "England and Wales Birth Registration Index, 1837-2008," database, FamilySearch(https://familysearch.org/ark:/61903/1:1:QV7G-NYZ2 : accessed 10 May 2016), Christiane M H Amanpour, 1958; from "England & Wales Births, 1837-2006," database, findmypast(http://www.findmypast.com : 2012); citing Birth Registration, Ealing, London, England, citing General Register Office, Southport, England.
  3. ABC News video: "Back to the Beginning: Bethlehem's Church of the Nativity" katika YouTube retrieved 10 August 2013 | Minute 6:06 | "My mother is a Christian from England and my father a Muslim from Iran. I married a Jewish American."
  4. Deborah White. "Profile of Christiane Amanpour, CNN Chief International Correspondent". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-25. Iliwekwa mnamo 24 August 2007.  Check date values in: |accessdate= (help)
  5. "Christiane Amanpour, CNN International Chief Correspondent". about.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-25. Iliwekwa mnamo 2019-10-16. 
  6. "Five Years Later, the Gulf War Story Is Still Being Told". New York Times. 12 May 1996.  Check date values in: |date= (help)
  7. "U S Exclusive Moammar Gadhafi Tells Christiane Amanpour that Libya's People Love Him ABC News". YouTube. Iliwekwa mnamo 29 July 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  8. Mike Allen (May 31, 2013). "Rubin, Amanpour to London". Politico. Iliwekwa mnamo October 8, 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  9. "CNN's Christiane Amanpour and Husband Jamie Rubin Are Divorcing After 20 Years". 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Christiane Amanpour kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.