Vita ya Bosnia
Vita ya Bosnia (1992–1995) ilikuwa mojawapo ya migogoro ya kikatili zaidi iliyowahi kutokea huko barani Ulaya tangu kwisha kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Vita hii ilitokea katika Jamhuri ya Bosnia na Herzegovina baada ya kuvunjika kwa Yugoslavia. Yugoslavia ilianza kuporomoka mwanzoni mwa miaka ya 1990 kutokana na mivutano ya kikabila na siasa za kujitenga kwa mataifa anuwai yaliyokuwa sehemu ya shirikisho hilo. Bosnia na Herzegovina ilikuwa ndiyo kambi kuu ya vikundi vitatu vya kikabila: Waislamu wa Bosnia (Bosniaks) – 44% ya idadi ya watu, Waserbia – 31%, na Wakroatia – 17%. Katika kura ya maoni ya mwaka 1992, Bosnia na Herzegovina ilitangaza kujitenga na mikononi mwa Yugoslavia, lakini Waserbia wa Bosnia walikataa matokeo hayo na walipinga kwa nguvu zote. Katika kufanikisha hili, walipata msaada kutoka katika serikali ya Serbia chini ya Rais Slobodan Milošević na Jeshi la Watu wa Yugoslavia (JNA). Punde walianza harakati za kijeshi ili kuhakikisha wanadhibiti maeneo makubwa ya Bosnia.
Vita vilianza rasmi mnamo Aprili 1992 baada ya Bosnia kutangazwa kuwa huru, na Waserbia wa Bosnia, wakiongozwa na Radovan Karadžić na vikosi vya Ratko Mladić. Walianzisha mashambulizi dhidi ya miji na vijiji vya Bosniaks na Wakroatia. Hali ya vita ilionyeshwa na mashambulizi yaliyokosa ubinadamu. Mauaji ya halaiki, na sera za "utakaso wa kikabila" ambapo Waserbia wa Bosnia walihamisha kwa nguvu au kuua jamii za Bosniaks na Wakroatia katika maeneo waliyotaka kudhibiti. Mashambulizi maarufu kama yale ya Srebrenica (1995), ambapo zaidi ya wanaume na wavulana wa Kibosnia 8,000 waliuawa, yalichukuliwa kuwa mauaji ya halaiki. Wakroatia wa Bosnia nao walipambana na Bosniaks kwa vipindi fulani, hasa mwaka 1993, huku wakiunda mamlaka yao huru iliyoitwa Herzeg-Bosnia. Migawanyiko hii ilichochea moto wa hali mbaya ya vita.
Jicho la dunia lilihamia Bosnia. Juhudi za usuluhishi wa kimataifa ziliendelea, lakini bila mafanikio. Umoja wa Mataifa ulipeleka walinda amani na kutangaza maeneo salama kama Srebrenica, lakini ulinzi huo haukufua dafu. Mwaka wa 1994, Marekani ilihusika katika kufanikisha makubaliano ya ushirikiano kati ya Bosniaks na Wakroatia, wakaunda Shirikisho la Bosnia na Herzegovina ili kupambana na Waserbia wa Bosnia. Mwishoni mwa 1995, baada ya mashambulizi ya NATO dhidi ya vikosi vya Waserbia wa Bosnia na shinikizo la kimataifa, viongozi wa pande zote walikutana mjini Dayton, Ohio, Marekani.
Vita vilimalizika kwa kusainiwa kwa Mkataba wa Dayton mnamo Desemba 14, 1995. Mkataba huu uliigawanya Bosnia na Herzegovina katika vipande viwili vikuu vya kiutawala: Shirikisho la Bosnia na Herzegovina (linalojumuisha Bosniaks na Wakroatia) na Jamhuri ya Srpska (eneo la Waserbia wa Bosnia). Serikali kuu iliundwa na vyombo vya pamoja vya utawala, huku mkataba ukilenga kudumisha amani na kuhakikisha uwakilishi wa makundi yote.
Baada ya vita, Bosnia na Herzegovina ilibaki katika hali ya udhaifu wa kiuchumi na kisiasa, huku maelfu ya watu wakiwa wakimbizi ndani na nje ya nchi. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita kwa Yugoslavia (ICTY) iliundwa ili kushughulikia uhalifu wa kivita uliofanywa wakati wa mgogoro, na viongozi kama Ratko Mladić na Radovan Karadžić walihukumiwa kwa mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita. Juhudi za maridhiano zilianza polepole, lakini hisia za kikabila bado zilikuwa kali.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Future of Bosnia and Hercegovina Balkan Insight
- "List of people missing from the war". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 3, 2009. Iliwekwa mnamo Juni 16, 2006.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - UN report on prison camps during the war
- Open UN document on Serb atrocities towards non-Serbs
- Summary of the ICTY verdicts related to the conflict between Bosnia and Herzegovina and the Federal Republic of Yugoslavia
- Summary of the ICTY verdicts related to the conflict between Bosnia and Herzegovina and Croatia
- Roy, Pinaki. "Bosnian War Requiems: Snippets of the Balkan Commemorations". The Atlantic Critical Review Quarterly. 10(4), October–December 2011. pp. 95–115. ISBN 978-81-269-1675-7, ISSN 0972-6373.
- Through My Eyes Website Imperial War Museum – Online Exhibition (Including images, video and interviews with refugees from the war in Bosnia)
- Map of Europe showing the Bosnian War (omniatlas.com)
- "Quest For War, and One Green Beret's Subsequent Evolution" contains insights on postwar activities by "Joint Commissioned Observers"
- Targeting History and Memory, SENSE – Transitional Justice Center (dedicated to the study, research, and documentation of the destruction and damage of historic heritage during the Balkan Wars of the 1990s. The website contains judicial documents from the International Criminal Tribunal for the former Yugoslavia (ICTY)).
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vita ya Bosnia kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |