Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya NBA

Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani (kwa Kiingereza: National Basketball Association au kifupi NBA) ni chama cha kitaifa cha timu za mpira wa kikapu zinazocheza katika ligi kuu huko Amerika ya Kaskazini ikijumuisha timu 29 toka Marekani na timu 1 toka Kanada. Ni moja ya ligi kubwa za kulipwa za mpira wa kikapu nchini Marekani na Kanada na ni ligi kubwa kabisa ya mpira wa kikapu duniani.

Ligi hii ilianzishwa huko New York City Juni 6, 1946, ikiitwa Chama cha Mpira wa Kikapu Amerika (BAA). Ilichukua jina lake la sasa Agosti 3, 1949 baada ya kuungana na mshindani wake Ligi ya Kitaifa ya Mpira wa Kikapu National Basketball League (NBL).

Msimu wa ligi hii huanza Oktoba na kumalizika Aprili, kila timu ikicheza michezo 82. Wachezaji wa ligi hii ni wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa duniani kwa kutazama wastani wa mshahara kwa mwaka.[1][2]

Chama hiki ni mwanachama wa USA Basketball (USAB),[3] chama kinachotambuliwa na [Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Kikapu]] (the International Basketball Federation - FIBA). Makao yake makuu yako Midtown Manhattan, wakati studio za NBA Entertainment na NBA TV ziko Secaucus, New Jersey.

Orodha ya timu za ukanda wa Mashariki (kwa Kiingereza: "Eastern Conference"):

 1. Atlanta Hawks
 2. Boston Celtics
 3. Charlotte Hornets
 4. Chicago Bulls
 5. Cleveland Cavaliers
 6. Detroit Pistons
 7. Indiana Pacers
 8. Miami Heat
 9. Milwaukee Bucks
 10. New Jersey Nets
 11. New York Knicks
 12. Orlando Magic
 13. Philadelphia 76ers
 14. Toronto Raptors
 15. Washington Wizards

Orodha ya timu za ukanda wa Magharibi (kwa Kiingereza: "Western Conference"):

 1. Dallas Mavericks
 2. Denver Nuggets
 3. Golden State Warriors
 4. Houston Rockets
 5. Los Angeles Clippers
 6. Los Angeles Lakers
 7. Memphis Grizzlies
 8. Minnesota Timberwolves
 9. New Orleans Pelicans
 10. Oklahoma City Thunder
 11. Phoenix Suns
 12. Portland Trail Blazers
 13. Sacramento Kings
 14. San Antonio Spurs
 15. Utah Jazz
Michezo ya video

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. "REVEALED: The world's best paid teams, Man City close in on Barca and Real Madrid". SportingIntelligence.com. May 1, 2012. Iliwekwa mnamo June 11, 2012.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
 2. Gaines, Cork. "The NBA is the highest-paying sports league in the world". Business Insider. Iliwekwa mnamo May 20, 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
 3. "Members of USA Basketball". USA Basketball. June 28, 2015. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo June 30, 2015. Iliwekwa mnamo June 28, 2015.  Check date values in: |date=, |archivedate=, |accessdate= (help)

Soma zaidi[hariri | hariri chanzo]


Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Ligi ina tovuti ya Kiingereza yenye mtazamo zaid wa kimataifa [1] yenye habari toka nje ya Marekani ya Kaskazini. Tovuti nyingine ni za Kiingereza zenye ushirikiano na vyombo vya habari nje ya Marekani kama vile Africa, Australia, Canada, India, New Zealand, na Philippines.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.