Uzuri
Uzuri ni sifa ya nafsi, mnyama, mahali, tendo, wazo, neno, tungo, sauti, picha au kitu chochote kinachopendeza.
Kimsingi, kwa wanaomuamini Mungu, ni sifa yake ambayo inajumlisha zile za umoja, ukweli na wema, na kujitokeza katika utakatifu wa watu wake.
Kwa namna mbalimbali uzuri unachunguzwa na falsafa, sosholojia, saikolojia n.k. na kulengwa na binadamu tangu zamani za kale, hasa kwa njia ya sanaa za aina mbalimbali. Tangu mtu yupo, hawezi kuridhika na mahitaji ya mwili tu.
Pengine uzuri unategemea utamaduni, lakini mara nyingi unapendeza watu wote.
Mang'amuzi ya "uzuri" mara nyingi yanatokana na utambuzi wa ulinganifu na uasilia, unaomfanya mtu ajisikie salama na kuridhika.
Hata hivyo, kwa kuwa mara kadhaa ni mang'amuzi ya binafsi, mithali ya Kiingereza inasema, "beauty is in the eye of the beholder" ("uzuri umo jichoni mwa mtazamaji")[1]hata pengine ni suala la urithi.[2][3]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Gary Martin (2007). "Beauty is in the eye of the beholder". The Phrase Finder. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-11-30. Iliwekwa mnamo Desemba 4, 2007.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ The Oxford Handbook for Aesthetics
- ↑ "Denis Dutton: A Darwinian theory of beauty | Video on TED.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-02-11. Iliwekwa mnamo 2014-09-22.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- BBC Radio 4's In Our Time programme on Beauty (requires RealAudio)
- Dictionary of the History of Ideas: Ilihifadhiwa 5 Machi 2005 kwenye Wayback Machine. Theories of Beauty to the Mid-Nineteenth Century
- beautycheck.de/english Ilihifadhiwa 13 Mei 2008 kwenye Wayback Machine. Regensburg University – Characteristics of beautiful faces
- Eli Siegel's "Is Beauty the Making One of Opposites?"
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |