Ulinganifu
Mandhari
Ulinganifu (pia: mpachano[1], ing. symmetry ) ni tabia ya maumbo na magimba yenye sehemu zinazolingana. Kama sehemu za kitu ni kama pacha zinaitwa linganifu.
Miili ya viumbehai wengi inafuata muundo wa ulinganifu kwa sababu macho, masikio, mikono, miguu na viungo vingine (si vyote!) viko mahali sawa upande wa kushoto kama upande wa kulia. Hii ni kama taswira geu inayoakisiwa. Mfuno huu unaweza kuitwa ulinganifu wa mstari[2] kwa sababu sehemu pacha ya geu inatokea kwenye mstari wa kioo au jira ya ulinganifu.
Kuna mfumo wa pili unaofuata nukta ya ulinganifu (pia: nukta ya pacha[3]). Hapo pande mbili zina umbali sawa na kitovu ambacho ni nukta ya ulinganifu.
Mifano ya maumbo linganifu
[hariri | hariri chanzo]-
Maumbo linganifu na jira za ulinganifu]]
-
Umbo lenye mfumo wa ulinganifu wa nukta ("Zentrum" = Kitovu")
-
Ulinganifu wa nukta kwamfano wa kiti cha pweza
-
Ulinganifu katika sanaa (mchoro wa Leonardo da Vinci)
-
Ulinganfu katika usanifu majengo
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Kujisomea
[hariri | hariri chanzo]- Stewart, Ian (2007). Why beauty is truth: the history of symmetry. Basic Books. ISBN 9780465082360.
Viungo ya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Calotta: A World of Symmetry
- Dutch: Symmetry Around a Point in the Plane Ilihifadhiwa 2 Januari 2004 kwenye Wayback Machine.
- Chapman: Aesthetics of Symmetry Ilihifadhiwa 25 Septemba 2017 kwenye Wayback Machine.
- ISIS Symmetry Ilihifadhiwa 22 Septemba 2009 kwenye Wayback Machine.
- International Symmetry Association – ISA Ilihifadhiwa 21 Julai 2006 kwenye Wayback Machine.
- Institute Symmetrion Ilihifadhiwa 21 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.