Nenda kwa yaliyomo

Alfajiri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfajiri huko Higuerote, Venezuela.

Alfajiri (kutoka Kiarabu فجر, fajir) ni kipindi cha siku ambacho kinaleta mwanga wa kwanza kabisa baada ya giza la usiku: wakati huo jua lenyewe halijaonekana, ila unaeleweka upande litakapotokea.

Kwa binadamu na wanyama wengi ndio wakati ambapo wanaelekea kutoka usingizini ili kuanza shughuli mbalimbali.

Katika dini mbalimbali, ni wakati muhimu wa sala, ili siku nzima na utendaji wake viongozwe na mwanga wa Mungu.

Katika Uislamu ni kipindi kimojawapo ambacho Waislamu wanaamrishwa kuswali ili wapate thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, tena ndiyo kipindi cha kwanza kati ya vitano vya sala vya kila siku, na ndio mwanzo wa saumu katika mwezi wa Ramadhani.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Alfajiri huko Taritari, Nueva Esparta, Venezuela Vipindi vya siku Kutwa huko Knysna, Afrika Kusini

UsikuUsiku katiUsiku wa mananeAlfajiriPambazukoAsubuhiAdhuhuriMchanaAlasiriJioniMachweo