Abuna Aregawi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanisa (awali nyumba ya Abuna Aregawi) huko monasteri ya Debre Damo.

Abuna Aregawi (pia: Za-Mika'el 'Aragawi au Mikaeli wa Aragave) alikuwa mmonaki wa karne ya 6, mfuasi wa Pakomi[1]. Anatajwa kama mwanzilishi wa monasteri ya Debre Damo katika jimbo la Tigray (Ethiopia), kwa agizo la mfalme Gebre Mesqel wa Axum[2].

Abba Aregawi anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 au 25 Oktoba.[3]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Ni kati ya Watakatifu Tisa wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia wanaosemekana kukimbilia nchi hiyo kutoka sehemu mbalimbali za Dola la Roma kutokana na dhuluma zilizofuata Mtaguso wa Kalsedonia (451). Wengine ni Abba Aftsé, Abba 'Aléf, Abba Gärima, Abba Guba, Abba Liqanos, Abba Pantelewon, Abba Sehma, Abba Yäm'ata (Yemata). Wote walikuwa wamonaki wasomi waliohuisha Ukristo wa Ethiopia. Wanasemekana kuwa ndio watafsiri wa Agano Jipya kwenda lugha ya Ge'ez.[4]

Baada ya kuishi miaka kumi na miwili katika ikulu mwa mfalme Ella Amida huko Axum, aliongozana na sista Edna kwenda Debre Damo. Baadaye mfalme Kalebu aliomba shauri kwake kabla hajaenda Arabia Kusini kupigana na mfalme Myahudi Dhu Nuwas.[5][6]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Michael Daniel Ambatchew, Tales of Abuna Aregawi, Publisher: Createspace Independent Pub (10 April 2006), ISBN|978-1419632693 Retrieved on 21 Mar 2018
  2. David Buxton, Travels in Ethiopia, second edition (London: Benn, 1957), p. 126
  3. "Debre Damo". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-01-29. Iliwekwa mnamo 2019-12-16. 
  4. Shinn, David H.; Ofcansky Bowen, Thomas P. (2013). Historical Dictionary of Ethiopia. United Kingdom: Scarecrow Press Inc. uk. 118. 
  5. "Biography of Zä-Mika'él 'Arägawi from The Dictionary of Ethiopian Biography". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-27. Iliwekwa mnamo 2019-12-16. 
  6. https://dacb.org/stories/ethiopia/za-mikael/


Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.