Abba Yamata

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Abba Yäm'ata)

Abba Yamata alikuwa mmonaki aliyefanya umisionari katika Ethiopia ya leo akaanzisha monasteri chini ya kanuni ya Pakomi huko Gar'alta[1].

Ni kati ya kundi la Watakatifu Tisa wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia wanaosemekana kukimbilia nchi hiyo kutoka sehemu mbalimbali za Dola la Roma[2] kutokana na dhuluma zilizofuata Mtaguso wa Kalsedonia (451). Wengine ni Abba Panteleoni, Abba 'Aléf, Abba Gärima, Abba Guba, Abba Liqanos, Abba Aregawi, Abba Sehma, Abba Aftse. Wote walikuwa wamonaki wasomi waliohuisha Ukristo wa Ethiopia. Wanasemekana kuwa ndio watafsiri wa Agano Jipya kwenda lugha ya Ge'ez.[3]

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Novemba.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. https://dacb.org/stories/ethiopia/yam-ata/
  2. The bishop Afonso Mendes, who had been the Roman Catholic Patriarch of Ethiopia under Emperor Susenyos, cited the "Chronicle of Axum" as saying about the Nine Saints, "In the days of Amiamid [i.e., Ella Amida] many monks came from Rum, who fill'd all the Empire; Nine of them stay'd in Tigre, and each of them erected a Church of his own Name." Cited in Tellez, The Travels of the Jesuits in Ethiopia, 1710 (LaVergue: Kessinger, 2010), pp. 89f.
  3. (2013) Historical Dictionary of Ethiopia. United Kingdom: Scarecrow Press Inc., 118. 
Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.