Abrahamu mkaapweke
Abrahamu mkaapweke (Edesa, leo Urfa, nchini Uturuki, 290 - Lapseki, 366) alikuwa mmonaki wa Mesopotamia katika karne ya 4 BK aliyetumwa kama padri mmisionari huko Beth-Kiduna; ndiyo sababu anaitwa Kidunaia.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 29 Oktoba[1].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa na familia tajiri akapewa mke akiwa bado kijana, lakini siku ya arusi alikimbia akajifungia katika chumba kisicho na mlango kwa miaka kumi. Hatimaye familia yake ilimruhusu kufuata wito wake.
Baadaye askofu alimpa upadrisho akamtuma kufanya umisionari katika mji uliokataa uongofu. Ingawa mwenyewe hakupenda hayo, kwa mwaka mmoja aliwaongoa wengi na kujenga kanisa.
Kwa sala zake alimuomba Mungu amtume mmisionari bora zaidi, na aliposikilizwa, alirudi upwekeni hadi mwisho wa maisha yake.
Alitoka mara moja tu, ili kumuongoa mtoto wa ndugu yake kutoka maisha maovu.
Maisha yake yaliandikwa na Efrem Mshamu[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |