Thomas More
Mtakatifu Thomas More (7 Februari, 1478 – 6 Julai, 1535) alikuwa mwanasheria kutoka Uingereza.
Ametambuliwa kuwa mtakatifu kama mfiadini.
Sikukuu yake ni tarehe 22 Juni kufuatana na kalenda rasmi ya Kanisa Katoliki, na 6 Julai katika Kanisa la Anglikana.
[hariri] Maisha
Thomas More alizaliwa katika mji wa London tarehe 7 Februari mwaka 1478.
Alisoma katika Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza, akaoa na kupata watoto wanne.
Aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mahakama wa Uingereza.
Aliandika vitabu kadhaa kuhusu mambo ya kiserikali, na vingine vya kutetea imani ya Kanisa Katoliki.
Pamoja na Mt. John Fisher alishindana na Mfalme Henri VIII kuhusu sUala la kuivunja ndoa ya huyo mfalme. Kwa amri ya Henri, wote wawili waliopinga kuvunjwa kwa ndoa yake walifungwa gerezani na kuuawa, kwanza John Fisher tarehe 22 Juni, halafu Thomas More tarehe 6 Julai, mwaka 1535.
[hariri] Tazama pia
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Thomas More kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |