Maria wa Bethania
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kristo nyumbani mwa Martha na Maria kadiri ya mchoro wa Johannes Vermeer (1654 hivi) unaotunzwa kwenye National Gallery of Scotland, Edinburgh. Maria ameketi miguuni pa Yesu.
Maria wa Bethania (jina lake kwa Kiebrania מִרְיָם, Miryām, kwa Kiaramu מרים, Maryām, kwa Kigiriki Μαρία, Maria) alikuwa mwanamke wa Bethania, kitongoji cha Yerusalemu. Ndugu zake walikuwa Martha na Lazaro wa Bethania.
Anajulikana hasa kutokana na Injili, kwa namna ya pekee Injili ya Luka na Injili ya Yohane, katika Agano Jipya ndani ya Biblia ya Kikristo. Humo anaonekana mwenye silika ya utulivu na imani kwa Yesu Kristo, ambaye alipendezwa sana na usikivu wake.
Anaheshimiwa na Wakristo wengi kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 4 Juni au 29 Julai, kadiri ya madhehebu.
Viungo vya nje [hariri]
- Easton's Bible Dictionary, 1897
- Catholic Encyclopedia 1910: under "Saint Mary Magdalene"
- Mary & Martha, the sisters of Lazarus, Greek Orthodox Archdiocese of America.
- CIRCULO SANTA MARIA DE BETANIA, group dedicated to the devotion of Saint Mary of Bethany in the Philippines
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Maria wa Bethania kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |