Martha wa Bethania
Martha wa Bethania (jina lake kwa Kiebrania na Kiaramu ni מַרְתָּא, Martâ, kwa Kigiriki Μαρθα, Martha) alikuwa mwanamke wa Bethania, kitongoji cha Yerusalemu. Ndugu zake walikuwa Maria na Lazaro wa Bethania.
Anajulikana hasa kutokana na Injili, kwa namna ya pekee Injili ya Luka na Injili ya Yohane, katika Agano Jipya ndani ya Biblia ya Kikristo. Humo anaonekana mwenye silika ya utendaji na imani kwa Yesu Kristo, ambaye alipendezwa na ukarimu wake, pamoja na kumuonya azingatie kwanza kilicho muhimu pekee.
Kisha kumkiri Yesu kuwa Kristo, Mwana wa Mungu aliyekuja ulimwenguni, alishuhudia alivyomfufua kaka yake Lazaro siku nne baada ya kifo chake.
Maneno yake kwa Yesu yalikuwa haya: "Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Lakini hata sasa najua ya kuwa yoyote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa... Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni". (Yoh. 11:21-22, 27)
Anaheshimiwa na Wakristo wengi kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 4 Juni au 29 Julai, kadiri ya madhehebu.
Viungo vya nje [hariri]
- "St. Martha, Virgin", Butler's Lives of the Saints
- St. Martha on catholic.org
- Mary & Martha, the sisters of Lazarus, Greek Orthodox Archdiocese of America
- Patron Saints: Martha
"St. Martha". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.- "The Life of Saint Martha", text from the Golden Legend
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Martha wa Bethania kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |