Ziwa Qinghai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ziwa Qinghai
Picha ya satelaiti mnamo Novemba 1994. Kaskazini iko upande wa kushoto.
Mahali Qinghai, China
Anwani ya kijiografia Coordinates: 37°00′N 100°08′E / 37.000°N 100.133°E / 37.000; 100.133
Aina ya ziwa Ziwa la chumvi
Eneo la maji km2 4186 (2004)
km2 4489(2007)[1]
Kina kikubwa m 32.8
Kimo cha uso wa maji juu ya UB m 3260
Visiwa Sand Island, Bird Islands
Miji mikubwa ufukoni Haiyan County
Marejeo [1]

Ziwa Qinghai ni ziwa kubwa zaidi nchini China. Iko katika Mkoa wa Qinghai uliopata jina lake kutoka kwa ziwa hili. Ziwa Qinghai ni ziwa la chumvi la magadi.

Majina[hariri | hariri chanzo]

"Qinghai" inamaanisha ziwa buluu. Ziwa hilo huwa na majina mbalimbali katika lugha za Kimongolia na Kitibeti yanayomaanisha "Ziwa la Buluu".

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Ziwa Qinghai liko karibu km 100 magharibi mwa Xining katika nyanda za juu za Tibet kwenye mita 3205 juu ya usawa wa bahari. [2] Lipo kati ya wilaya za Haibei na Hainan za Tibet kaskazini mashariki mwa jimbo la Qinghai katika kaskazini magharibi ya China.

Eneo la ziwa limeonekana kubadilika; limepungua wakati wa karne ya 20 lakini limeongezeka tangu 2004. Mnamo mwaka 2008 ziwa lilikuwa na eneo la km2 4217. Kina cha wastani ni m 21.[3]

Mito 23 huingia ndani ya Ziwa Qinghai lakini hakuna njia ya maji kutoka, isipokuwa kwa uvukizaji. Kwa njia hiyo ziwa limezidi kuwa ziwa la chumvi lenye magadi mengi. Kwa sasa ziwa huwa na asilimia 14 za chumvi.

Tabianchi[hariri | hariri chanzo]

Uso wa mji huganda na kuwa barafu wakati wa majira ya baridi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Area of Qinghai Lake Has Increased Continuously. China Council for International Cooperation on Environment and Development. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-08-28. Iliwekwa mnamo 2019-11-06.
  2. Buffetrille 1994, p. 2; Gruschke 2001, pp. 90 ff.
  3. Zhang, Guoqing (2011). "Water level variation of Lake Qinghai from satellite and in situ measurements under climate change". Journal of Applied Remote Sensing 5: 053532. doi:10.1117/1.3601363. 

Vitabu[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ziwa Qinghai kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.