Ziwa Balkhash

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ziwa Balkhash
Picha ya satelaiti mnamo Aprili 1991
Ramani ya beseni ya Ziwa Balkhash
Mahali Kazakhstan
Anwani ya kijiografia Coordinates: 46°10′N 74°20′E / 46.167°N 74.333°E / 46.167; 74.333
Aina ya ziwa Ziwa la chumvi
Mito ya kuingia mito ya Ili, Karatal, Aksu, Lepsy, Byan, Kapal, Koksu
Mito ya kutoka uvukizaji
Nchi za beseni Kazakhstan 85%
China 15%
Urefu km 605
Upana Mashariki km 19, magharibi km 74
Eneo la maji km2 16400
Kina cha wastani m 5.8
Kina kikubwa m 26
Mjao km3 106
Kimo cha uso wa maji juu ya UB m 341.4
Huganda Novemba hadi Machi

Ziwa Balkhash (kwa Kikazakhi: Балқаш көлі, Balqaş kóli; kwa Kirusi: Озеро Балхаш, Ozero Balkhash) ni moja ya maziwa makubwa zaidi barani Asia na ziwa kubwa la tano duniani. Liko katika Asia ya Kati, mashariki mwa Kazakhstan ndani ya beseni linaloshirikiwa na Kazakhstan na China, pamoja na sehemu ndogo ya Kirgizia. Beseni halina njia ya maji kutoka nje.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Maji huingia ndani ya ziwa kupitia mito saba ilhali mkubwa ni Mto Ili. Chanzo cha maji ni usimbisaji hasa kutoka kwa kuyeyuka kwa theluji kwenye milima ya jimbo la Xinjiang wa China .

Ziwa kwa sasa linajumuisha eneo la karibu km2 16400. Walakini, kama Ziwa Aral maji yake huzidi kupungua kama matokeo ya kupunguka kwa maji kutoka mito inayolilisha. [1]

Ziwa limegawanywa na shingo nyembamba kwa sehemu mbili tofauti. Sehemu ya magharibi ni maji safi, wakati nusu ya mashariki ni ya chumvi. [2] [3] [4] [5] Sehemu ya mashariki iko kwa wastani kubwa mara 1.7 zaidi kuliko sehemu ya magharibi.

Mji mkubwa karibu na ziwa pia unaitwa Balkhash na una wenyeji wapatao 66,000. Shughuli kubwa za kiuchumi katika eneo hilo ni pamoja na uchimbaji madini na uvuvi.

Wakati ukubwa wa ziwa hilo unaongezeka kwa muda, kuna wasiwasi juu ya kuzidi kwa ziwa kwa sababu ya jangwa na shughuli za viwandani.

Tabianchi[hariri | hariri chanzo]

Mji wa Balkhash
Jedwali la tabianchi (maelezo)
J
F
M
A
M
J
J
A
S
O
N
D
 
 
13
 
 
−9
−18
 
 
10
 
 
−8
−18
 
 
10
 
 
0
−10
 
 
11
 
 
14
3
 
 
15
 
 
22
10
 
 
12
 
 
28
16
 
 
10
 
 
30
18
 
 
8
 
 
28
16
 
 
4
 
 
22
9
 
 
9
 
 
13
2
 
 
14
 
 
3
−6
 
 
15
 
 
−5
−13
Halijoto wastani ya juu na chini kwa °C
Usimbisaji jumla kwa mm

Masuala ya mazingira na ya siasa[hariri | hariri chanzo]

Kuna wasiwasi mkubwa juu ya mazingira ya ziwa, hasa kwa kukumbuka matatizo ya mazingira katika Ziwa Aral ambalo limegeuzwa kuwa jangwa kutokana na machafuko na matumizi ya maji yake. [6]

Tangu mwaka 1970, km3 39 matumizi ya maji kujaza Bwawa la Kapchagay yalisababisha kupungua kwa 2/3 kwa maji yaliyoingia ziwani kutoka Mto Ili. [2] Uso wa maji ziwani ulishuka kila mwaka sentimita 15.6[7].

Kushuka kwa maji ya Balkhash kunaonekana sana katika sehemu yake ya magharibi na kusababisha pia kupotea kwa maziwa madogo karibu nayo.[8] Kati ya maziwa madogo 16 ya ziwa iliyopo karibu na maziwa matano tu ndiyo yaliyobaki. Mchakato wa kuenea kwa jangwa uliathiri karibu 1/3 ya beseni lake. [9] Vumbi la chumvi limepulizwa mbali na kuchangia kutokea kwa dhoruba za vumbi katika sehemu za Asia, kuongezeka kwa chumvi ya udongo na kuathiri vibaya hali ya hewa.

Ekolojia ya bonde la Ili-Balkhash inaathiriwa pia na uchafuzi wa hewa kutokana na viwanda ambako madini yanayeyushwa, hasa kwenye Kiwanda cha Madini cha Balkhash. Katika miaka baada ya 1990, uzalishaji wa metali mbalimbali ulipeleka tani 280-320,000 kwa mwaka hewani, pamoja na tani 76 za shaba, tani 68 za zinki na tani 66 za plumbi kuteremka kwenye uso wa ziwa.[10]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Lake Balkhash, International Lake Environment Committee
  2. 2.0 2.1 Lake Balkhash. Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 2009-01-29.
  3. Igor S. Zektser, Lorne G Everett (2000). Groundwater and the Environment: Applications for the Global Community. CRC Press, 76. ISBN 1-56670-383-2. 
  4. Maria Shahgedanova (2002). The Physical Geography of Northern Eurasia. Oxford University Press, 140–141. ISBN 0-19-823384-1. 
  5. Yoshiko Kawabata (1997). "The phytoplankton of some saline lakes in Central Asia". International Journal of Salt Lake Research 6 (1): 5–16. doi:10.1007/BF02441865 .
  6. You must specify title = and url = when using {{cite web}}. (Russian). UNDP Kazakhstan (4 November 2004). Jalada kutoka ya awali juu ya 22 July 2011. Iliwekwa mnamo 2009-02-14.
  7. Water resources of Kazakhstan in the new millennium (Russian). UNDP Kazakhstan (April 19, 2004). Jalada kutoka ya awali juu ya March 6, 2007. Iliwekwa mnamo 2009-02-14.
  8. Guillaume Le Sourd, Diana Rizzolio (2004). United Nations Environment Programme – Lake Balkhash. UNEP Global Resource Information Database. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-08-18. Iliwekwa mnamo 2009-01-29.
  9. N. Borovaya (4 October 2005). Спасти уникальное озеро. Стремительно мелеет казахстанский Балхаш (Russian). Экспресс К, No. 186 (15844). Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-07-18. Iliwekwa mnamo 2009-01-29.
  10. A. Samakova (2005-10-01). The main problem of Balkhash Lake is poor water quality (Russian). zakon.kz. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-03-07. Iliwekwa mnamo 2009-01-29.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ziwa Balkhash kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.