Yellowstone National Park

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yellowstone National Park

Grand Canyon of the Yellowstone
MahaliUnited States
  • Park County, Wyoming
  • Teton County, Wyoming
  • Gallatin County, Montana
  • Park County, Montana
  • Fremont County, Idaho
Eneoacre 2 219 791 (ha 898 318)
Kuanzishwa1, 1872 (1872-March-01)
Visitors4,115,000 (in 2018) [1]
Mamlaka ya utawalaU.S. National Park Service
Tovuti[http:// Official website]
Mto Yellowstone kwenye tambarare

Hifadhi ya Taifa ya Yellowstone ni mbuga ya kitaifa nchini Marekani. Ilikuwa mbuga ya kwanza wa kitaifa kutangazwa duniani. [2]

Jina lilichukuliwa kutoka Mto Yellowstone, ambao unapita katikati ya hifadhi. Yellowstone lilipokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO mwaka 1978.

Hifadhi ya Taifa ya Yellowstone ni maarufu kwa geyser zake na chemchemi za moto. Hifadhi hiyo ina karibu nusu ya geyser zote duniani. [2] Geyser maarufu inaitwa Old Faithful kwa sababu inachemka kwa umakini mkubwa kia baada ya dakika ama 65 au 91. Kuna wanyamapori aina za dubu, mbwa mwitu, baisani na elki. Watalii wengi hutembelea mbuga hiyo kila mwaka kuona geyser na wanyama huko.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Karibu asilimia 96 ya mbuga ziko katika jimbo la Wyoming. Asilimia tatu ziko Montana na asilimia moja tu huko Idaho. Eneo lake ni km2 9,100. .

Miaka 640,000 iliyopita Yellowstone ilikuwa mahali pa volkeno kubwa.

Volkeno hii ilisababishwa na " hotspot " katika koti ya Dunia, ambako bamba la Amerika Kaskazini lilipita juu yake na kuyeyusha ganda la Dunia hapa. Mlipuko mkubwa wa volkeno ulirusha kilomita za mjazo 1,000 za miamba na lava hewani. cubic mile 240 (km3 1 000) ya mwamba na lava angani.[3]

Wataalamu wanategemea kutokea kwa mlipuko mwingine katika muda usio mbali sana.[4]

Swala la Pronghorn hupatikana mahali pengi kwenye nyasi za mbuga.

Baisoni[hariri | hariri chanzo]

Baisoni hutafuta malisho karibu na chemchemi ya moto

Kati ya wanyama wakubwa mashuhuri wa Yeloowstone ni kundi la baisoni. Hao ng'ombe mwitu wakubwa walijaza nyika za Amerika ya kaskazini kwa idadi za mamilioni hadi karne ya 19. Mwaka 1902 wanyama 50 waliokuwa kati ya mwisho waliobaki walipelekwa Yellowstone. Mnamo mwaka 2003 idadi yao ilikuwa imeongezeka kufikia 4,000.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kigezo:NPS visitation
  2. 2.0 2.1 "UNESCO, Yellowstone National Park". UNESCO. Iliwekwa mnamo 2012-04-19. 
  3. "Tracking changes in Yellowstone's restless volcanic system". U.S. Geological Survey. 2006-01-09. Iliwekwa mnamo 2007-03-12. 
  4. Lowenstern, Jake (June 2005). "Truth, fiction and everything in between at Yellowstone". Geotimes (American Geologic Institute). Iliwekwa mnamo 2007-03-12.  Check date values in: |date= (help)

Tovuti zingine[hariri | hariri chanzo]