Wastara Juma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wastara Juma Issa (maarufu kama Wastara Juma; alizaliwa mkoani Morogoro, nchini Tanzania, 27 Septemba 1983) ni mwigizaji wa filamu za Kitanzania (Bongo movies).

Elimu yake[hariri | hariri chanzo]

Wastara Juma alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Mvomero A katika miaka ya 1989 - 1995 mkoani Morogoro. Alijiunga na elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Agricalture mkoani Morogoro mnamo mwaka 1996. [1]

Kutokana na kushindwa kuendelea na elimu ya sekondari, mwaka 1997, Wastara alifanikiwa kupata mume aliyejulikana kwa jina la Juma Issa ambapo mwaka 1998 alibahatika kuzaa naye mtoto mmoja kisha ndoa hiyo ikasambaratika kutokana na kutofautiana kwa tabia.

Maisha ya uwigizaji[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kuvutiwa na kazi mbalimbali alizokuwa akizifanya mwigizaji na mchekeshaji anaejulikana kwa jina la, Athuman Majuto ‘King Majuto’, mwaka 1999 Wastara alianza rasmi sanaa ya maigizo na filamu yake ya kwanza kucheza iliitwa Utaishia kunawa akiwa na gwiji wa vichekesho nchini hayati King Majuto. Mnamo miaka ya 2004 - 2006 alianza kuonekana kwenye mchezo wa Miale uliokuwa unarushwa na kituo cha televisheni cha ITV.

Mwanzoni mwa mwaka 2007, Wastara alifanya usahili na kufanikiwa kuigiza filamu iliyojulikana kama elemende kisha zikafuata filamu nyingine kama Penina kabla ya kutimkia nchini Kongo kufanya biashara. [2]

Mnamo Julai 2007 Wastara alirejea kutoka Kongo sanjari na kuitwa na mwigizaji Shija ambaye alimuomba aigize naye filamu baada ya kumuona kupitia kazi mbalimbali alizowahi kufanya hapo nyuma. Huu ndio mwanzo wa Wastara kukutana na Juma Kilowoko (Sajuki) ambaye baadae wakawa wapenzi baada ya kutambua kuwa wote wawili walikuwa na matatizo sawa katika mapenzi yaani kutendwa. Wawili hawa katika umoja wao walifanikiwa kuporomosha filamu zaidi ya 20 ikiwemo Mboni.

Mwaka 2009, wiki moja kabla ya ndoa yake, alipata ajali ya pikipiki akiwa na mumewe ambayo ilimsababishia Wastara kukatwa mguu, lakini hii haikubadilisha ndoto ya wao kuoana kwa sababu walifunga ndoa wakiwa katika kiti cha wagonjwa.[3]

Baada ya hapo, Wastara na Sajuki walianzisha kampuni yao ya Wa-Jey na kuendelea kuzalisha filamu kama Briefcase, The Killers, Seven Days na nyinginezo.

Tarehe 2 Januari 2013) Wastara alimpoteza mume wake jambo lililosababisha kupumzika sanaa kwa muda na baadae alirejea kwenye tasnia na kutoa filamu ya Shaymaa amabayo ilipata umaarufu mkubwa.

Filamu alizowahi kuigiza[hariri | hariri chanzo]

Gumzo | Doctor Max | Njia Panda | Shaymaa | Mr & Mrs Sajuki | Kivuli | Kozopata | Kijacho | Detective | Liganga | Nzowa | The Killers | Vivian | Vita | Briefcase | Mchanga na Keni | Peremende | Round | Mboni Yangu |[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]