Utamaduni wa Nok

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo ambalo mabaki ya utamaduni wa Nok yamepatikana katika Nigeria.
Sanamu ya Nok, terakota, Louvre, Ufaransa.

Utamaduni wa Nok ulikuwa ustaarabu wa kale katika maeneo ya Nigeria ya sasa. Ulitokea mnamo mwaka 1000 KK na kutoweka mnamo 300 BK.

Ustaarabu huo ulitambuliwa kutokana na mabaki yake ya kiakiolojia kaskazini na katikati mwa Nigeria.

Jina linatokana na kijiji cha Nok katika Jimbo la Kaduna ambako sanamu zilitambuliwa mnamo 1968 wakati wa uchimbaji katika migodi. Ufundi na ubora wa sanaa ulionyesha hali ya utamaduni wa juu, utafiti wa ardhi ambako sanamu zilikutwa ulithibitisha ni mabaki ya siku kabla ya kuzaliwa kwa Kristo. Utafiti wa udongo ulionyesha pia sanamu zote zilizopatikana katika eneo kubwa zilifinyangwa kwa udongo wa eneo moja dogo; hivyo wachunguzi walihisi eneo hilo lilikuwa na namna ya utawala au serikali ya pamoja.

Mfumo wake wa kijamii unadhaniwa kuwa uliendelea sana kwa wakati wake. Wasanii wa Nok wanaaminiwa kuwa wazalishaji wa kwanza wa sanamu ukubwa wa maisha za terakota (udongo uliochomwa) katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Wataalamu wamependekeza kuwa watu wa Nok walikuwa watangulizi wa Wayoruba wa leo. [1] [2] Walitumia chuma katika zana za kuyeyusha na kughushi kuanzia angalau mwaka 550 KK, na labda mapema zaidi. [3] [4] [5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Chambers Encyclopaedia New Revised Edition, vol. 10, p 40, International Learning Systems Corporation Ltd London
  2. The New Universal Library, vol. 14, p 456. The Caxton Publishing Company London
  3. Jared Diamond, 'Guns, Germs, and Steel: The Fates of Human Societies' (1997) Chapter 19
  4. Duncan E. Miller and N.J. Van Der Merwe, 'Early Metal Working in Sub Saharan Africa' Journal of African History 35 (1994) 1-36
  5. Minze Stuiver and N.J. Van Der Merwe, 'Radiocarbon Chronology of the Iron Age in Sub-Saharan Africa' Current Anthropology 1968. Tylecote 1975 (see below)
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Utamaduni wa Nok kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.