Tutuko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tutuko
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyInfectious diseases, dermatology Edit this on Wikidata
ICD-10A60., B00., G05.1, P35.2
ICD-9054.0, 054.1, 054.2, 054.3, 771.2
DiseasesDB5841 33021
eMedicinemed/1006
MeSHD006561

Tutuko (kutoka kitenzi "kututuka"; pia Hepesi simpleksi kutoka jina la Kiingereza lenye asili ya Kigiriki ἕρπης, herpes, "unaoenea polepole" au "uliofichika") ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya hepesi simpleksi.[1]

Maambukizi yameainishwa kulingana na sehemu ya mwili iliyoambukizwa. Hepesi ya mdomo hujumuisha uso au mdomo. Inaweza kusababisha malengelenge madogo katika vikundi yaitwayo vidonda baridi au malengelenge ya joto jingi au inaweza tu kusababisha maumivu ya koo.[2][3] hepesi ya viungo vya uzazi ambayo inaweza kuwa na dalili chache au kusababisha malengelenge ambayo hupasuka na kusababisha vidonda vidogo. Hivyo kwa kawaida hupona kwa muda wa wiki mbili hadi nne. Maumivu yanayowasha au yanayochoma yanaweza kutokea kabla ya malengelenge kutokea. Hepesi huzunguka kati ya vipindi vya ugonjwa vilivyo na dalili vikifuatiwa na vipindi visivyo na dalili. Kwa kawaida kipindi cha kwanza huwa kali zaidi na kinaweza kuhusishwa na joto jingi, maumivu ya misuli, nodi ya limfu iliyovimba na maumivu ya kichwa. Muda unavyosonga, vipindi vya ugonjwa vilivyo na dalili hupungua kwa mara unapotokea na ukali.[1]

Matatizo mengine yanayosababishwa na hepesi simpleksi hujumuisha: paronikia ya hepesi inapohusisha vidole,[4] hepesi ya macho,[5] maambukizi ya hepesi ya ubongo,[6] na hepesi ya watoto wachanga inapoathiri mtoto mchanga, n.k.[7]

Kisababishi na utambuzi[hariri | hariri chanzo]

Kuna aina mbili za virusi vya hepesi simpleksi: aina ya 1 (HSV-1) na aina ya 2 (HSV-2).[1] HSV-1 kwa kawaida zaidi husababisha maambukizi ya mdomo huku HSV-2 kwa kawaida zaidi ikisababisha maambukizi ya viungo vya uzazi.[2]

Husababishwa kwa kugusana moja kwa moja kwa viowevu vya mwili au vidonda vya mtu aliyeambukizwa. Kuenea bado kunaweza kutokea hata iwapo dalili hazipo. Hepesi ya jenitalia imeainishwa kama maambukizi yanayoenezwa kupitia ngono. Yanaweza kuenezwa kwa mtoto mchanga wakati wa kuzaliwa.[1] Baada ya kuambukizwa, maambukizi husafirishwa kupitia nyuroni inayopitisha hisia hadi kwa seli za neva, pale ambapo virusi hukaa kwa maisha yote.[2]

Visababishi vya kujirudia vinaweza kujumuisha: kupungua kwa utenda kazi wa kingamwili, mafadhaiko na kupatana na jua.[8][2]

Hepesi ya mdomo na ile ya jenitalia kwa kawaida hutambuliwa kwa kuzingatia dalili zilizodhihirika.[2] Utambuzi unaweza kuthibitishwa na tabia ya virusi au DNA ya kutambua hepesi kwenye viowevu vinavyotoka katika malengelenge. Kuchunguza damu ili kutambua kingamwili dhidi ya virusi kunaweza kuthibitisha maambukizi ya hapo awali lakini kutakuwa hasi katika maambukizi mapya.[1]

Kinga na tiba[hariri | hariri chanzo]

Njia inayofaa zaidi ya kuzuia maambukizi ya viungo vya uzazi ni kwa kuzuia ngono kupitia uke, mdomo, au unyeo. Matumizi ya kondomu yanaweza kupunguza, lakini si kuondoa hatari. Dawa ya kila siku ya kudhibiti virusi inayonywewa na mtu aliyeambukizwa pia inaweza kuzuia kuenea. Hakuna chanjoinayopatikana.

Unapoambukizwa hakuna tiba.[1] Paracetamol (acetaminophen) na topical lidocaine zinaweza kutumika ili kupunguza dalili.[2] Matibabu kwa dawa za kudhibiti virusi kama vile asiklovia au valasiklovia yanaweza kupunguza ukali wa vipindi vinavyodhihirisha dalili.[1][2]

Uenezi[hariri | hariri chanzo]

Viwango vya HSV 1 au HSV-2 ulimwenguni kote ni kati ya asilimia 60 na 95 kwa watu wazima.[9] HSV-1 kwa kawaida hupatikana utotoni.[1] Viwango vya zote huongezeka watu wanapozeeka.[9] Viwango vya HSV-1 huwa kati ya asilimia 70 na 80 katika watu ambao hali yao ya kijamii na kiuchumi ni ya chini na asilimia 40 hadi 60 kwa watu ambao hali yao ya jijamii na kiuchumi imeboreka.[9] Kadirio la watu milioni 536 ulimwenguni kote (asilimia 16 ya watu) walikuwa wameambukizwa HSV-2 kufikia 2003 huku viwango vya juu zaidi vikiwa wanawake na walio katika ulimwengu unaoendelea.[10] Watu wengi walio na HSV-2 hawatambui kuwa wameambukizwa.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 1.8 "Genital Herpes - CDC Fact Sheet". cdc.gov. December 8, 2014. Iliwekwa mnamo 31 December 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 Balasubramaniam, R; Kuperstein, AS; Stoopler, ET (April 2014). "Update on oral herpes virus infections.". Dental clinics of North America 58 (2): 265–80. PMID 24655522.  Check date values in: |date= (help)
  3. Mosby (2013). Mosby's Medical Dictionary (toleo la 9). Elsevier Health Sciences. ku. 836–837. ISBN 9780323112581. 
  4. Wu, IB; Schwartz, RA (March 2007). "Herpetic whitlow.". Cutis 79 (3): 193–6. PMID 17674583.  Check date values in: |date= (help)
  5. Rowe, AM; St Leger, AJ; Jeon, S; Dhaliwal, DK; Knickelbein, JE; Hendricks, RL (January 2013). "Herpes keratitis.". Progress in retinal and eye research 32: 88–101. PMID 22944008.  Check date values in: |date= (help)
  6. Steiner, I; Benninger, F (December 2013). "Update on herpes virus infections of the nervous system.". Current neurology and neuroscience reports 13 (12): 414. PMID 24142852.  Check date values in: |date= (help)
  7. Stephenson-Famy, A; Gardella, C (December 2014). "Herpes Simplex Virus Infection During Pregnancy.". Obstetrics and gynecology clinics of North America 41 (4): 601–614. PMID 25454993.  Check date values in: |date= (help)
  8. Elad S; Zadik Y; Hewson I n.k. (August 2010). "A systematic review of viral infections associated with oral involvement in cancer patients: a spotlight on Herpesviridea". Support Care Cancer 18 (8): 993–1006. PMID 20544224. doi:10.1007/s00520-010-0900-3. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-09-15. Iliwekwa mnamo 2016-11-01.  Unknown parameter |= ignored (help); Check date values in: |date= (help)
  9. 9.0 9.1 9.2 Chayavichitsilp P, Buckwalter JV, Krakowski AC, Friedlander SF (April 2009). "Herpes simplex". Pediatr Rev 30 (4): 119–29; quiz 130. PMID 19339385. doi:10.1542/pir.30-4-119.  Check date values in: |date= (help)
  10. Looker, KJ; Garnett, GP; Schmid, GP (October 2008). "An estimate of the global prevalence and incidence of herpes simplex virus type 2 infection.". Bulletin of the World Health Organization 86 (10): 805–12, A. PMC 2649511. PMID 18949218. doi:10.2471/blt.07.046128.  Check date values in: |date= (help)