Nenda kwa yaliyomo

TAZARA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Tazara)
Treni ya TAZARA kwenye kituo cha Mlimba
Kituo cha TAZARA huko Dar es Salaam
Kituo cha TAZARA huko Ifakara

TAZARA (kifupi cha Tanzania Zambia Railway) ni shirika la pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Zambia, lililoanzishwa mnamo mwaka 1975.

Lengo kuu la TAZARA ni kuendesha huduma za reli kati ya bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania na kituo cha New Kapiri Mposhi iliyopo kwenye njia ya reli kati ya Lusaka na Kitwe kwenye ukanda wa shaba wa Zambia, ikipitia eneo la kati la Tanzania na Zambia. Reli hii inachukua jukumu muhimu katika usafirishaji wa abiria na mizigo kati ya Tanzania na Zambia, na pia inachangia katika kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Njia ya TAZARA

Njia ya TAZARA ina urefu wa kilomita 1,860. Njia ya reli ina upana sawa na reli za Zambia na Afrika Kusini lakini ni tofauti na njia za Reli ya Tanzania hivyo treni na magari hayawezi kutumiwa pande zote nchini Tanzania.

Reli ilianza kazi yake mwaka 1976 kwa mashine 120 lakini sasa ziko 30 pekee hasa za makampuni za Krupp na General Electric. Mashine asilia za Kichina haziendi tena.

Idadi ya mabehewa inazidi 2,000 kuna mabehewa 100 za abiria. Kwa jumla utunzaji wa njia, mebehewa na mashine ilikuwa tatizo katika historia ya TAZARA.

Vituo muhimu vya TAZARA ni pamoja na:

Muda wa safari kwa treni ya haraka ni masaa 40, takriban 25 upande wa Tanzania na takriban 15 upande wa Zambia. Kwa jumla mwendo wa treni ni polepole sana.

Shabaha ya mradi wa kujenga TAZARA

Ukaguzi wa awali wa njia ya reli ulianza mwaka 1968. Hatua hii ilikuwa kutazamia mahali ambapo reli itapita. Ujenzi wa reli ya TAZARA iliuanza kuanzia mwaka 1970 hadi 1976 Julai na Jamhuri ya Watu wa China kama zawadi kwa mataifa ya Zambia na Tanzania. Ujenzi ulitekelezwa na wafanyakazi Wachina zaidi ya 20,000.

Shabaha ya mradi ilikuwa hasa kisiasa ililenga kuanzisha usafiri kwa ajili ya shaba ya Zambia usiotegemea mabandari ya Afrika Kusini na Msumbiji. Msumbiji wakati ule ilikuwa koloni ya Ureno na Afrika Kusini ilitawaliwa kwa mfumo wa apartheid (siasa ya ubaguzi wa rangi). Zambia chini ya serikali ya Kenneth Kaunda iliunga mkono upinzani dhidi ya apartheid na ukoloni ikaona aibu ya kutegemea nchi hizi kiuchumi. China ilitaka kuimarisha msimamo kati ya mataifa huru ya Afrika ikajitolea kujenga reli kwa kuipa Zambia njia nyingine ya kufikia bahari.

Viungo vya Nje