Shirika la Reli Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Shirika ya Reli Tanzania)
Jump to navigation Jump to search
Njia za reli za TRC
Treni ya TRC katika kituo cha reli Daressalaam
Kituo cha reli Kigoma

Shirika la Reli Tanzania au Tanzania Railways Limited (TRL - hadi 2007 TRC [1]) ni kampuni ya umma inayoendesha usafiri kwenye mtandao mkubwa zaidi wa reli nchini Tanzania.

Boriti ya chuma ya mwaka 1912 kwenye njia ya reli ya Kigoma mwaka 2012

Inaendesha hasa usafiri kwenye njia za reli zifuatazo katika Tanzania

Hali ya shirika ilikuwa duni mno na tangu miaka mingi njia ya kaskazini haina huduma ya abiria. Kuna mipango ya kuboresha huduma.

TRC ni tofauti na kampuni ya TAZARA inayoendesha reli kati ya Daressalaam na Zambia.

Historia[hariri | hariri chanzo]

TRC inatumia njia za reli zilzoanzishwa wakati wa ukoloni katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na kupanuliwa wakati wa utawala wa Kiingereza. Kabla na baada ya uhuru shirika la East African Railways and Harbours Corporation ilitawala reli za Tanzania, Kenya na Uganda. Mwaka 1977 shirika hili lilivunjwa pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa ajili ya reli na mabandari katika Tanzania TRC ilianzishwa. Hali ya reli iliendelea kushuka polepole kutokana na utawala mbaya. Majaribio kadhaa za kufufusha kampuni yalishindikana.

Mwaka 2007 shirika la TRC lilivunjwa likaisha kumiliki njia za reli pamoja na kuwajibika kwa usafiri hapa pamoja na mawasiliano kwa mabasi ya reli.

Mwaka 2007 shughuli za kuendesha usafiri wa reli ilihamishwa kwa shirika jipya la "Tanzania Railways Limited" (TRL) iliyokuwa mradi wa pamoja wa serikali ya Tanzania na kampuni ya RITES kutoka nchini Uhindi. Tangu mwaka 2011 Jamhuri ya Maungano ya Tanzania imeshika hisa zote (100%) za TRL.[2].

Mtandao wa reli ulibaki mkononi mwa serikali ikimilikiwa na Reli Assets Holding Company Ltd (RAHCO) kama wakala wa serikali.[3]

Njia za reli[hariri | hariri chanzo]

TRC imerithi njia zenye upana wa mita 1 kwa urefu wa kilomita 2,600. Usafiri wote ni kwa injini za diseli.

Leo hii injinitreni na mabehewa ni bovu, hali ya njia ya reli pia kwa hiyo treni zinazoendelea kusafiri hutembea polepole na kwa kuchelewa. Ratiba ya safari kati ya Daressalaam hadi Kigoma ni masaa 40 kwa kilomita 1252 inayolingana na mkasi wa 30 km/h. Zamani kulikuwa na terni 3 za abiria kila wiki, lakini mwaka 2011 hali halisi ilikuwa treni 1 pekee.

Mabehewa ya kwenda Mwanza yanasafiri pamoja na treni ya Kigoma na kuwa treni ya pekee huko Tabora.

TRL na TAZARA[hariri | hariri chanzo]

Upana wa njia ya TRL ni tofauti na TAZARA kwa hiyo mabehewa hayawezi kuingia kutoka njia ya kampuni moja kwa nyingine. Daressalaam na Kidatu kuna vituo vya huhamishia mizigo kati ya makampuni haya.

Mipango ya njia mpya Tanga - Musoma - Uganda[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka 2011 kuna mapatano kati ya Tanzania na Uganda kuanzisha njia ya reli mpya kati ya Tanga na Kampala kupitia Arusha na feri kwenye Ziwa Viktoria.[4]

Kufuatana na mapatano haya kilomita 400 kati ya Tanga na Arusha zitaboreshwa na njia mpya ya kilomita 480 kutengenezwa kutoka Arusha kwenda Musoma. Kwenye bandari ya Musoma mizigo itahamishwa kwenye feri kwenda Uganda. sehemu ya mipango hii ni ujenzi wa bandari mpya huko Tanga - Mwambani na bandari mpya huko Kampala - Bukasa.

Njia hii mpya itakuwa fupi kuliko njia zilizopo kwa sasa kati ya pwani la Bahari Hindi na Uganda.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Hadi 2007 Tanzania Railways Corporation (TRC)
  2. TRL - "Background". Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-11-16. Iliwekwa mnamo 2016-09-28.
  3. Tovuti ya RAHCO[dead link]
  4. Taarifa ya East African. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-10-17. Iliwekwa mnamo 2015-10-17.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]