Sigismundi wa Bourgogne

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Sigismundi alivyochorwa ukutani na Piero della Francesca, 1451.

Sigismundi wa Bourgogne (alifariki Saint-Maurice-en-Valais, leo nchini Uswisi, 524) alikuwa mfalme wa Burgundy tangu mwaka 516 hadi alipouawa na wapinzani wake[1].

Anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Mei[2].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kuongokea Kanisa Katoliki kutoka Uario kwa msaada wa Avito wa Vienne[3], alianzisha monasteri mahali pa kifodini cha Morisi Mtakatifu na Kikosi cha Thebe ambapo wamonaki wamuimbie Mungu sifa mfululizo[4].

Baada ya kurithi ufalme, alimuua mwanae, akatubu kosa hilo kwa machozi mengi na kufunga chakula.

Hatimaye alishindwa vitani na Wafaranki akafungwa akauawa pamoja na familia yake yote.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Gábor Klaniczay, Holy Rulers and Blessed Princesses: Dynastic Cults in Medieval Central Europe, (Cambridge University Press, 2000), 67–68. ISBN|0-521-42018-0
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
  3. John Bagnell Bury, History of the Later Roman Empire: From the Death of Theodosius I to the death of Justianian, Vol. I, (Dover Publications, 1958), 463.
  4. Perennial Prayer at Agaune, Barbara H. Rosewein, Monks and Nuns, Saints and Outcasts, ed. Lester K. Little, Sharon A. Farmer and Barbara H Rosenwein, (Cornell University Press, 2000), 39–40. ISBN|0-8014-3445-9

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.