Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Nembo la FAO

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (Ing. Food and Agriculture Organzation of the United Nations (FAO)) ni kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachopambana na tatizo la njaa duniani.

Inalenga kuboresha uzalishaji na ugawaji wa mazao na vyakula duniani kwa shabaha ya kuboresha hali ya malisho ya watu duniani.

FAO iliundwa tar. 16 Oktoba 1945 mjini Québec nchini Kanada. 1951 makao makuu yalihamshwa kwenda Roma, Italia. Mwaka 2007 nchi 191 pamoja na Umoja wa Ulaya zilikuwa wanachama. Tangu 1981 siku ya 16 Oktoba hukumbukwa kila mwaka kama "Siku ya Chakula Duniani".

Shughuli za FAO ziko hasa za aina nne:

  1. FAO inawasilisha mawasiliano kati ya wataalamu kwenye uwanja wa lishe na chakula. Inaajiri wataalamu wa kilimo, bilojia, misitu, uvuvi na ufugaji. Inaendesha semina na warsha ya kimataifa ambako watalaamu wanakutana na kubadilishana habari na mawazo. Tovuti ya FAO inakusanya habari husika na inatembelewa zaidi ya mara milioni kila mwezi.
  2. FAO inatuma washauri katika nchi nyingi wanaosaidia kupanga siasa ya kilimo.
  3. FAO inakutanisha serikali za nchi nyingi katika maswala ya lishe na kilimo.
  4. FAO inakusanya ujuzi kwa kazi ya kila siku, inaongoza au kushauri miradi mielfu ya kilimo kote duniani. Pamoja na Mradi wa Lishe Duniani inasaidia pia katika maeneo penye njaa kwa kuleta msaada wa haraka kwa watu wasio na chakula.

Ofisi za FAO[hariri | hariri chanzo]

Ofisi za kanda[hariri | hariri chanzo]


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]