Raimundi wa Penyafort
Mandhari



Raimundi wa Penyafort, O.P., (kwa Kikatalunya Sant Ramon de Penyafort; kwa Kihispania San Raimundo de Peñafort, Vilafranca del Penedès, Catalonia, 1175 hivi; Barcelona, 6 Januari 1275) alikuwa padri maarufu kwa utaalamu wake katika masuala ya sheria.
Mkusanyo wake wa sheria za Kanisa Katoliki uliendelea kuwa wa msingi hata karne ya 20. Pia aliandika vizuri sana kuhusu sakramenti ya kitubio[1].
Aliongoza shirika la Wahubiri na kulipatia katiba mpya; pia alisaidia kuanzisha lile la Wamersedari.
Papa Paulo III alimtangaza mwenye heri mwaka 1542 na Papa Klementi VIII kuwa mtakatifu tarehe 29 Aprili 1601.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Januari[2][3].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ "Calendarium Romanum" (Libreria Editrice Vaticana, 1969), pp. 85 and 114
- ↑ Martyrologium Romanum
Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk 12-13
- Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 9-10
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- [1] Katika Catholic Encyclopedia
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |