Rafka Petra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha halisi ya Mt. Rafka Petra akiwa mahututi kitandani.

Rafka Petra Choboq Ar-Rayès, O.L.M. (kwa Kiarabu: رفقا بطرسيّة شبق ألريّس; Himlaya, 29 Juni 1832Jrebta, 23 Machi 1914), alikuwa mwanamke mmonaki wa Kanisa la Wamaroni nchini Lebanon.

Baada ya kujiunga la masista walimu alichukua nafasi ya kujifungia monasterini kwa maisha ya sala na toba zaidi, ambayo yaliendana na upofu kwa miaka 30 na maumivu mengi ya kiafya aliyoyapokea na kuyatoa kama sadaka akimtegemea Mungu tu.

Bikira huyo alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 16 Novemba 1985, halafu mtakatifu tarehe 10 Juni 2001.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.