Pumeza Matshikiza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pumeza Matshikiza (* 1979) ni mwimbaji mwenye sauti ya soprano kutoka nchini Afrika Kusini.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa mnamo mwaka 1979 katika jimbo la Rasi ya Mashariki na wazazi Waxhosa. Waliachana alipokuwa mdogo na mama yake alihamia Jimbo la Rasi pamoja naye. Hapo waliishi katika mitaa ya vibanda mbalimbali karibu na mji wa Cape Town.

Pumeza aliimba katika kwaya kanisani akapenda muziki. Alipokuwa na umri wa miaka 15 alisikia mara ya kwanza uimbaji wa opera kwenye redio akavutwa na aina hii ya muziki. Alipokuwa na umri wa miaka 20 aliweza kuhudhuria maonyesho ya opera mara ya kwanza.

Wakati wa kumaliza shule alishauriwa kusoma upimaji wa ramani akaanza somo hili lakini baada ya muda alihamia chuo kikuu cha muziki cha Capetown kwa somo la uimbaji. Baada ya kumaliza mwaka 2004 alipata nafasi ya kuendelea kwenye Royal College of Music mjini London na kwenye chuo cha wasanii vijana kwenye Royal Opera House, Covent Garden.[1]

Mwaka 2011 alipata ajira kweye nyumba ya opera ya Stuttgart nchini Ujerumani.[2]

Mwaka 2014 alitoa albamu yake ya kwanza alipounganisha uimbaji wa opera na nyimbo za Kixhosa na Kiswahili.[3]

Mwaka 2014 Pumeza aliimba mbele ya umati mkubwa wakati wa ufunguzi wa michezo ya Jumuiya ya Madola mjini Edinburgh nchini Uskoti.[4]

Albamu[hariri | hariri chanzo]

Albamu yake ya kwanza ilitolewa na kampuni ya Decca kwa jina Pumeza - Voice of Hope

1. "O mio babbino caro" - aria of Gianni Schicchi, all arias with Staatsorchester Stuttgart, Simon Hewett
2. "Signore, ascolta!" aria of Liù from Turandot
3. Thula Baba (Hush, My Baby)
4. Malaika (My Angel)
5. Pata Pata
6. The Naughty Little Flea
7. "Vedrai, carino" aria of Zerlina from Don Giovanni
8. "Donde lieta uscì" aria of Mimi from La Boheme
9. Umzi Watsha
10. Saduva (Hush I Hear You)
11. Holilili
12. The Click Song
13. Iya Gaduza
14. Lakutshon Ilanga (When The Sun Sets) with the Royal Liverpool Philharmonic Orchestra, Iain Farrington
15. Freedom Come All Ye - Pumeza Matshikiza, Sura Susso, Mamadou Ndiaye Cissokho, Fiona Hamilton, Phil Cunningham

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

  • [[1]] Tovuti ya Pumeza mwenyewe

Marejeo[hariri | hariri chanzo]