Pergamon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mfano mdogo wa mji wa Kale
Altari ya Pergamon jinsi ilivyosimamishwa katika makumbusho ya Berlin

Pergamon (jina la leo Kituruki Bergama; Kigiriki: Πέργαμον; Kilatini: Pergamum) ilikuwa mji wa Ugiriki ya Kale kwenye pwani la magharibi la Asia Ndogo katika Uturuki ya leo. Leo hii uko hapa mji wa Bergama takriban kilomita 80 kaskazini ya Izmir.

Wakati wa karne ya 3 na 2 kabla ya Kristo Pergamon ilikuwa mji mkuu wa milki iliyotawala sehemu kubwa za Asia Ndogo. Watawala wa nasaba ya Attalos walipamba mji kwa mahekalu na taasisi zilizoufanya kitovu cha utamaduni wa Kigiriki.

Pergamon ilikuwa na maktaba kubwa ya pili katika dunia ya Mediteranea baada ya maktaba ya Aleksandria, inasemekana maktaba hii ilikuwa na vitabu vya miswada 200,000.

Mfano mashuhuri wa utamaduni huu ni altari kubwa iliyochukuliwa kutoka maghofu ya Pergamon na wajerumani wakati wa karne ya 19 na kupelekwa Berlin ambako makumbusho ya pekee ilijengwa kwa ajili ya altari hii.

Watu wa Pergamon[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: