Maktaba ya Aleksandria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Maktaba jinsi ilivyoonekana zamani

Maktaba ya Aleksandria ilikuwa maktaba kubwa na mashuhuri ya zama za kale. Ilianzishwa mjini Aleksandria katika Misri wakati wa utawala wa mfalme Ptolemayo I (305–283/82 KK). Ptolemayo alikuwa jenerali mgiriki chini ya Aleksander Mkuu aliyeendelea kutawala Misri na kujitangaza kama mfalme. Alichagua Aleksandria kama mji mkuu mpya na kupamba mji kwa majengo na taasisi mengi.

Wakuu wa maktaba walikuwa wataalamu mashuhuri kama Eratosthenes ambao mara nyingi walikuwa pia walimu wa wana wa mfalme.

Maktaba ililenga kukusanya vitabu vyote vilivyopatikana. Serikali ya Misri iliagiza ya kwamba kila mgeni alipaswa kuonyesha vitabu na miandiko yake yote vilichunguliwa na maafisa wa maktaba na kama havikuwemo bado vilinakiliwa haraka. Hata jahazi zilizoingia katika bandari zilitembelewa na maafisa wa maktaba na vitabu vyote kuchunguliwa kama lazima kukamatwa na kunakiliwa.

Mwanahistoria Mroma Aulus Gellius aliandika ya kwamba maktaba ilikuwa na vitabu 700,000 wakati wa Julius Caesar.

Vitabu vingi viliharibiwa wakati wa vita kati ya Caesar na Kleopatra.

Hakuna uhakika maktaba iliendelea kwa muda gani baada ya uharibifu huo.