Nenda kwa yaliyomo

Pergamon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Pergamo)
Mfano mdogo wa mji wa kale
Altari ya Pergamon jinsi ilivyosimamishwa katika makumbusho ya Berlin

Pergamon (jina la leo kwa Kituruki Bergama; kwa Kigiriki: Πέργαμον; kwa Kilatini: Pergamum) ilikuwa mji wa Ugiriki ya Kale kwenye pwani ya magharibi ya Asia Ndogo katika Uturuki ya leo. Leo hii uko huko mji wa Bergama takriban kilomita 80 kaskazini ya Izmir.

Wakati wa karne ya 3 na ya 2 kabla ya Kristo Pergamon ilikuwa mji mkuu wa milki iliyotawala sehemu kubwa za Asia Ndogo. Watawala wa nasaba ya Attalos walipamba mji kwa mahekalu na taasisi zilizoufanya kitovu cha utamaduni wa Kigiriki.

Pergamon ilikuwa na maktaba kubwa ya pili katika dunia ya Mediteranea baada ya maktaba ya Aleksandria: inasemekana maktaba hii ilikuwa na vitabu vya miswada 200,000.

Mfano mashuhuri wa utamaduni huu ni altari kubwa iliyochukuliwa na Wajerumani kutoka maghofu ya Pergamon wakati wa karne ya 19 na kupelekwa Berlin ambako makumbusho ya pekee yalijengwa kwa ajili ya altari hii.

Pergamon inatajwa na kitabu cha Ufunuo katika Agano Jipya (Biblia ya Kikristo) kama mahali pa Kanisa lililoandikiwa barua kwa njia ya Mtume Yohane (2:12-17).

Watu wa Pergamon

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: