Paramaribo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Paramaribo
Nchi Surinam
Nyumba za kale za Waholanzi huko Paramaribo.
Mahali pa Paramaribo katika Surinam.

Paramaribo (jina fupi: Par'bo) ni mji mkuu wa Surinam.

Iko kando ya mto Surinam takriban km 20 kutoka mwambao wa Bahari ya Karibi. Anwani ya kijiografia ni 5°52' N, 55°10' W.

Ina wakazi 250,000, karibu nusu ya wakazi wa nchi.

Kiini cha mji huo kimeorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia mwaka 2002.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Jina la Paramaribo limetokana na kijiji cha wakazi asilia "Parmirbo". Mwaka 1613 Waholanzi walijenga kituo cha biashara karibu na kijiji hicho. Mwaka 1651 eneo lilikuwa chini ya utawala wa Uingereza waliojenga hapa Fort Willoughby. Waholanzi walirudi mwaka 1667 wakatwaa eneo lote na kuita kituo Fort Zeelandia na kijiji mbele yake "Nieuw Middelburgh". Mwaka 1683 nyumba 27 zilihesabiwa zilizoongezeka hadi mwaka 1790 kuwa zaidi ya 1000.

Mji wa kale ulichomwa moto mara mbili (1821 na 1832).

Baada ya mwisho wa utumwa mwaka 1863 wengi waliowahi kuwa watumwa walihamia mjini na kusababisha kukua kwa Paramaribo. Tangu mwaka 1975 imekuwa mji mkuu wa Surinam huru.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Biashara ya nje kutoka Paramaribo ni hasa boksiti, sukari, mpunga, kokoa, kahawa na ubao. Kuna viwanda vya saruji, rangi na bia.

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Utamaduni wa Paramaribo una pande nyingi kutokana na mchanganyiko wa watu wenye asili ya Uhindi, Afrika, Indonesia, Uchina na Ulaya.

Wenyeji wanapenda mashindano ya uimbaji wa ndege wanaofugwa kwa kusudi hilo. Mashindano hayo hutokea kila Jumapili.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Paramaribo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.