Nyenje-ardhi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyenje-ardhi
Nyenje madoa-mawili (Gryllus bimaculatus)
Nyenje madoa-mawili (Gryllus bimaculatus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Orthoptera (Wadudu wenye mabawa nyofu)
Nusuoda: Ensifera (Wadudu kama nyenje)
Familia ya juu: Grylloidea (Nyenje)
Familia: Gryllidae (Nyenje-ardhi)
Laicharting, 1781
Ngazi za chini

Vikundi vya nusufamilia 2, nusufamilia 13 (10 katika Afrika):

Nyenje-ardhi ni wadudu wa familia Gryllidae katika oda Orthoptera. Wadudu hao ni tofauti na nyenje-miti ambao wamo katika Cicadoidea (Hemiptera). Nyenje-ardhi wanafanana kidogo na panzi lakini mabawa yao yanajifunga bapa mgongoni, vipapasio ni virefu sana na kama nyuzi na hawaruki mbali sana kwa kawaida. Licha ya jina lao kuna spishi zinazoishi mitini, zile za Oecanthinae hasa.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Nyenje-ardhi ni wadudu wadogo hadi wa ukubwa wastani wenye miili ya umbo la mcheduara iliyo bapa kidogo. Wana wakubwa wa familia ni nyenje-fahali wa urefu wa sm 5 (Brachytrupes) ambao huchimba penyo za kina cha mita moja au zaidi. Nyenje wadogo sana wanapitia sm 1 kidogo tu.

Kichwa kina umbo la mviringo chenye vipapasio virefu na vyembamba vilivyo juu ya skapi (pingili za kwanza) za umbo la koni na nyuma ya hizi ni macho makubwa mawili ya sehemu nyingi. Kwenye paji la uso kuna oseli tatu (macho sahili). Pronoto (pingili ya kwanza ya toraksi) ina umbo la tenge, ni ngumu na ina deraya ya khitini. Ni laini na haina mikuku juu yake wala kwenye pande zake.

Ncha ya fumbatio ina jozi ya serki ndefu (jozi ya viambatisho kwenye pingili ya mwisho) na majike pia wana mrija mrefu kwa kutaga mayai (oviposito). Mrija huo unaweza kuwa mnyofu na mwembamba kama sindano au uliopindika na mpana zaidi kama kitara. Femuri (pingili za tatu) za miguu ya nyuma zimekuwa kubwa sana kwa kusudi ya kuruka. Tibia (pingili za nne) ya miguu ya nyuma zina vipi kadhaa kama kingo vinavyoweza kusogea. Mpangilio wa vipi hivyo ni maalumu kwa kila spishi. Tibia za miguu ya mbele hubeba timpano moja au kadhaa, viwambo vya kupokea sauti. Nyenje hutofautiana na vikundi vingine vya Ensifera kwa kuwa na tarsi zenye pingili tatu badala ya nne.

Mabawa yapo bapa juu ya mwili na yanatofautiana sana kwa ukubwa kati ya spishi. Hupunguka kwa ukubwa katika nyenje kadhaa na hukosekana kwa wengine. Mabawa ya mbele ni elitro zilizotengenezwa na khitini ngumu. Zinafanya kama ngao ya kinga kwa sehemu nyororo za mwili na kwa madume hubeba viungo vya kutetema kwa uzalishaji wa sauti. Walakini mabawa ya mbele ya nyenje-mti ni mororo na mangavu. Mabawa ya nyuma ni kama viwambo na yanakunjika chini ya mabawa ya mbele kama kipepeo. Katika spishi nyingi mabawa hayakutoholewa kwa kuruka angani.

Uzazi na mzunguko wa maisha[hariri | hariri chanzo]

Hatua za nyenje: A. Dume akipiga sauti. B. Jike wenye mrija wa kutaga. C. Tunutu. D. Jike akiingiza omrija wa kutaga ardhini. E. Jike akitaga mayai.

Madume wa nyenje huanzisha utawala dhidi ya wenzao kwa uchokozi. Wanaanza kwa kupigiliana na vipapasio vyao na kutanua mandibulo zao. Isipokuwa mmojawapo ajirudie wakati huu, wanaishia kugombana, wakitoa kila mmoja kititi milio iliyo tofauti kabisa na ile iliyopigwa katika hali nyingine. Wakati mmojawapo anafikia utawala huimba kwa sauti kubwa, huku anayeshindwa akae kimya. Kwa ujumla majike huvutiwa na madume kwa milio yao, ingawa katika spishi zisizopiga mlio lazima utaratibu mwingine ushirikishwe. Baada ya wenzi kufanya mawasiliano kwa vipapasio, kipindi cha uchumba kinaweza kutokea wakati sifa ya mlio hubadilika. Jike hupanda dume na spermatoforo (kibumba chenye manii) huhamishwa kwenye viungo vya uzazi vya nje vya jike. Manii hutiririka kutoka kwa hiyo kuelekea kwenye ovidukiti ya jike kwa kipindi cha dakika chache au hadi saa moja kulingana na spishi. Baada ya kupandana jike anaweza kuondoa au kula spermatoforo lakini dume anaweza kujaribu kuzuia hii kwa tabia anuwai za kidesturi. Jike huweza kupandana mara kadhaa na madume wengine.

Nyenje wengi sana hutaga mayai yao kwenye mchanga au ndani ya mashina ya mimea na kufanya hivyo, majike wa nyenje wana chombo kirefu, kama sindano au kama kitara, kinachotumika kutaga mayai na kinachoitwa oviposito. Spishi fulani zinazokaa ardhini zimepoteza hiki na hutaga mayai yao ama kwenye chumba chini ya ardhi au kuyasukuma dhidi ya ukuta wa upenyo. Nyenje mkia-mfupi (Anurogryllus) huchimba upenyo mwenye vyumba na eneo la kunya, hutaga mayai yake katika rundo kwenye sakafu ya chumba na baada ya mayai kutoa tunutu, huwalisha kwa karibu mwezi moja.

Nyenje ni wadudu wenye metamofosisi isiyo kamili ambao mzunguko wa maisha yao una hatua ya yai, hatua za tunutu ambaye anazidi kufanana na maumbile ya mpevu wakati anapokua, na hatua ya mpevu. Yai hutoa tunutu wa takriban ukubwa wa nzi-matunda mdogo. Huyu hupita karibu na hatua 10 za tundu na baada ya kila uambuaji ufuatao anakuwa zaidi kama mpevu. Baada ya uambuaji wa mwisho viungo vya uzazi na mabawa yamekua kabisa, lakini kipindi cha kukomaa kinahitajika kabla nyenje ni tayari kuzaliana.

Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]