Kiambatisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kiambatisho (kutoka kitenzi cha Kibantu kuamba, kikiwa na mnyambuliko kuambata; kwa Kiingereza: attachment) ni chochote kinachoambatanishwa na barua.

Katika utarakilishi ni jalada linalotumwa kwenye barua pepe. Kwa mfano, kiambatisho kinawezesha kushirikisha picha, filamu au nakala.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Petzell, M. (2005). Expanding the Swahili vocabulary. Africa & Asia, 5, 85-107.