Nenda kwa yaliyomo

Nikanori Ascanio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro rasmi wa wafiadini 11 wa Damasko.

Nikanori Ascanio, O.F.M. (Villarejo de Salvanes, Hispania, 10 Januari 1814 - Damasko, Syria, 10 Julai 1860) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Waoservanti na padri wa Kanisa Katoliki aliyeuawa na Wadruzi kwa sababu alikataa kusilimu[1].

Pamoja naye waliuawa Wafransisko wenzake 7: mapadri 5 (Manuel Ruiz, Karmelo Bolta, Engelbati Kolland, Petro Nolasko Soler, Nikola Maria Alberca) na mabradha 2 (Fransisko Pinazo na Yohane Yakobo Fernandez) na ndugu 3 wa Kanisa la Wamaroni (Fransisko, Abdel Mooti na Rafaeli).

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini tangu tarehe 20 Oktoba 2024, alipotangazwa na Papa Fransisko. Kabla ya hapo alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI tarehe 10 Oktoba 1926.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • (Kiitalia) Guido Pettinati, I Santi canonizzati del giorno, vol. VII, edizioni Segno, Udine 1991, pp. 113-120.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.