Nenda kwa yaliyomo

Musa Mwafrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Musa Mwafrika.

Musa Mwafrika, maarufu pia kama Musa Mwizi (330405), alikuwa mmonaki padri nchini Misri na mmojawapo kati ya mababu wa jangwani.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakristo wa madhehebu mengi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Julai katika Ukristo wa Mashariki na tarehe 28 Agosti katika Ukristo wa Magharibi[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Mzaliwa wa Ethiopia[2], Musa alikuwa mtumishi wa afisa wa serikali nchini Misri mpaka alipofukuzwa kwa thuhuma za kuiba na kuua.[3]

Akiwa jitu, akawa bosi wa kundi la majambazi lililotisha watu wa bonde la Nile kwa ukatili.

Alipojaribu kukwepa waliokuwa wanamwinda, alifichama kwa wamonaki wa jangwani huko Wadi El Natrun (Sketes), karibu na Alexandria. Juhudi za kiroho, utulivu na furaha walivyokuwa navyo vilimuathiri kwa dhati. Muda mfupi baadaye aliacha mtindo wake wa kuishi, akabatizwa na kujiunga na monasteri ile.[4]

Kwanza alipata shida sana kuzoea nidhamu ya jumuia ile. Alipovamiwa na wezi chumbani mwake, aliwazidi nguvu akawaburuza hadi katika kikanisa walimokuwemo wenzake wakisali ili aambiwe awafanyie nini wageni hao.

Musa alikuwa na ari katika yote aliyoyafanya, lakini alikata tamaa alipojitambua si mkamilifu kutosha. Hapo abati Isidori alimchukua alfajiri hadi juu ya paa ili kutazama miali ya kwanza ya jua. Halafu akamuambia, "Taratibu tu miali ya jua inaondoa usiku na kuleta mchana mpya, na vilevile taratibu tu mtu anakuwa mwanasala kamili."[3]

Baadaye Musa akawa mwenyewe kiongozi wa jumuia ya wakaapweke katika sehemu nyingine ya jangwa, wakiwemo wenzake wa zamani[5], akapewa upadrisho.[3]

Alipokuwa na umri wa miaka 75 hivi, ilisikika kwamba kundi la Waberber limepanga kushambulia monasteri yao. Wenzake walitaka kujihami, lakini Musa aliwazuia akawaambia ni afadhali wakimbie kuliko kushika silaha. Mwenyewe na wengine 7 walibaki hadi walipouawa tarehe 1 Julai.[4][6]

Kwa sababu hiyo Musa Mwafrika anaheshimiwa leo kama mtetezi wa msimamo wa kukataa silaha katika kudai haki.[7]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Martyrologium Romanum
  2. "Venerable Moses the Black of Scete", Orthodox Church in America
  3. 3.0 3.1 3.2 "History of St. Moses the Black Priory". Stmosestheblackpriory.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-08-29. Iliwekwa mnamo 2014-02-14.
  4. 4.0 4.1 "Moses The Black", Again Magazine, pp. 28-30, June 1994
  5. https://www.santiebeati.it/dettaglio/67925
  6. A different story of Abba (Father) Moses' death is related in The Paradise of the Holy Fathers: 31. Abba Poemen said: Abba Moses asked Abba Zechariah a question when he was about to die, and said unto him, "Father, is it good that we should hold our peace?" And Zechariah said unto him, "Yea, my son, hold thy peace." And at the time of his death, whilst Abba Isidore was sitting with him, Abba Moses looked up to heaven, and said, "Rejoice and be glad, O my son Zechariah, for the gates of heaven have been opened."The Paradise Or Garden of the Holy Fathers: Being Histories of the ... - Saint Athanasius (Patriarch of Alexandria) - Google Boeken. Books.google.com. Iliwekwa mnamo 2014-02-14.
  7. "St. Moses the Black A Patron Saint of Non-Violence By Pieter Dykhorst « In Communion". Incommunion.org. 2011-12-07. Iliwekwa mnamo 2014-02-14.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.