Msinduzi
Msinduzi | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Msinduzi (Croton talaeporos) ni mti wa nusufamilia Crotonoideae katika familia Euphorbiaceae. Unatokea pwani ya Kenya na Somalia ya Kusini katika misitu wazi na nyika yenye miti au vichaka.
Maelezo[1]
[hariri | hariri chanzo]Spishi hii ni kichaka au mti mdogo wa urefu wa m 2-10. Gome lake ni kijivu na lina nyufa. Majani yana umbo la yai pana, msingi mviringo au wa umbo la moyo, ncha kali au butu, ukingo wenye meno ya mviringo, sm 4-16 kwa 3-15, yenye nywele chache lakini baadaye bila nywele. Maua ni meupe au njano iliyofifia yenye urefu wa mm 2-3, yenye jinsia moja au mbili, katika vishada vya urefu wa sm 8-20 (yote ya kiume au ya jinsia zilizochanganywa). Matunda mekundu au kahawia, karibu umbo la donge au ndewe tatu, mm 20-28 kwa 22-25 mm, yenye nywele.
Matumizi
[hariri | hariri chanzo]Mizizi hutumika kama dawa ya mafua na ya malalamiko ya tumbo.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Beentje, H.J. (1994) Kenya trees, shrubs and lianas. National Museums of Kenya, Nairobi.