Mkate wa uzima

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa ukutani wa mwanzoni mwa karne ya 3 ukionyesha mkate wa ekaristi na samaki, Katakombu wa Mt. Kalisti, Roma, Italia.

Mkate wa uzima (kwa Kigiriki ἄρτος τῆς ζωῆς, artos tēs zōēs) ni mojawapo kati ya namna saba ya Yesu Kristo kujitambulisha katika Injili ya Yohane kwa kutanguliza "Mimi ndimi..."[1].

Yesu alijiita hivi baada ya kuzidisha mkate na samaki kwa umati wa watu waliomfuata.

Lengo la muujiza huo halikuwa tu kutuliza njaa yao, bali kudokeza karamu ya mbinguni ambayo itashibisha hamu zote za binadamu kwa utimilifu wa uzima.

Hotuba hiyo inapatikana katika Yoh 6:22-59 ambamo imeandikwa kuwa ilitolewa katika sinagogi la Kapernaumu.[2]

Pamoja na kwamba Injili hiyo haisimulii jinsi Yesu alivyowaachia wanafunzi wake mwili na damu yake katika maumbo ya mkate na divai wakati wa karamu ya mwisho, inazungumzia fumbo la ekaristi hasa katika sehemu ya mwisho ya hotuba hiyo, ikisisitiza kuwa Yesu amejifanya chakula kweli na kinywaji kweli[3].

Kwa njia yake tu mtu anaweza kuwa na uzima wa Kimungu (Yoh 5:26)[4].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Who Do You Say That I Am?: Essays on Christology by Jack Dean Kingsbury, Mark Allan Powell, David R. Bauer 1999 ISBN 0-664-25752-6 page 83
  2. The Gospel According to John: A Literary and Theological Commentary by Thomas L. Brodie 1997 ISBN 0-19-511811-1 page 266
  3. The Eucharist in the New Testament by Jerome Kodell 1988 ISBN 0-8146-5663-3 page 118
  4. The Person of Christ by Gerrit Cornelis Berkouwer 1954 ISBN 0-8028-4816-8 page 163
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkate wa uzima kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.