Mawazine

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mawazine
Mawazine

Mawazine (Kiarabu: موازين‎) ni tamasha la kimataifa la Morocco inayofanyika kila mwaka huko Rabat, Morocco, ikiwashirikisha wasanii wengi wa muziki wa kimataifa na wazawa. Tamasha hili inaongozwa na Mounir Majidi, katibu wa mfalme wa Morocco, Mohammed VI na mwanzilishi na raisi wa utamaduni wa Maroc, taasisi inayoratibu Mawazine na tamasha zingine.[1] Watu takribani milioni 2.5 walihudhuria tamasha la Mawazine mwaka 2013 na kuifanya kuwa tamasha kubwa zaidi duniani baada ya Donauinselfest huko Viena.[2] [3]

Wasanii kama Whitney Houston, Mariah Carey, Rod Stewart, Charles Aznavour, Stevie Wonder, Alicia Keys, Shakira, Rihanna, Justin Timberlake, Jennifer Lopez, Enrique Iglesias, Demi Lovato, Christina Aguilera, Ricky Martin, Pharrell Williams, Iggy Azalea, Bruno Mars, Wiz Khalifa, Pitbull, Kanye West, Scorpions, La Fouine, Maître Gims, Damso, Booba, French Montana, Usher, Avicii, Akon, David Guetta, DJ Snake, Hardwell, Placebo, The Chainsmokers, Maroon 5, The Jacksons, Sugababes, Chic, Evanescence, Chris Brown, Luis Fonsi, Nick Jonas, Stromae, Jason Derulo, Juanes, Lenny Kravitz, The Weeknd, Kylie Minogue, Ellie Goulding, Sting, Julio Iglesias, Ennio Morricone, Robert Plant, Cat Stevens, B.B. King, Susana Baca, Carlos Santana, Elton John, Deep Purple and Travis Scott wamekwisha tumbuiza katika tamasha la Mawazine.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Vivarelli, Nick (19 February 2014). "Justin Timberlake to Open Morocco's Mawazine Music Fest". Variety.  Check date values in: |date= (help)
  2. "The 10 biggest music festivals in the world", MTVIGGY, 2013-05-24. 
  3. "Deadly stampede at Rabat festival", BBC News, 2009-05-24.