Nenda kwa yaliyomo

Mariah Carey

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mariah Carey
Mariah Carey, mnamo Mei 2013
Mariah Carey, mnamo Mei 2013
Maelezo ya awali
Amezaliwa 27 Machi 1969 (1969-03-27) (umri 55)[1]
Aina ya muziki R&B, pop, hip hop,[2] dance[3]
Kazi yake Singer, songwriter, model, record producer, actress
Aina ya sauti Alto[4]
Miaka ya kazi 1988–hadi sasa
Studio Columbia, Virgin, MonarC, Island
Tovuti www.mariahcarey.com

Mariah Carey (alizaliwa 27 Machi 1969) ni mwanamuziki, mtunzi, mtayarishaji na mwigizaji wa Marekani.

Alitengeneza albamu yake iliyofanya vizuri katika masoko mbalimbali na chati mbalimbali mwaka 1990, chini ya studio ya Columbia Records chini ya Tommy Mottola na kuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike kufikisha wimbo katika nafasi ya kwanza nchini Marekani. Hii ikiwa ni chati ya Billboard Hot 100. Baada ya kuolewa na Mttola mwaka 1993, mfululizo wa nyimbo bora zilimfanya moja kati ya wanamuzki bora wa Columbia na pia alikuwa anaongoza katika mauzo ya albamu mbalimbali. Kwa mujibu wa gazeti la Billboard Carey alikuwa mwanamuzi mwenye mafanikio zaidi katika miaka yab 1990 nchini Marekani [5]

Kufuatia kuachana na Mottola mwaka 1997, Carey alianza kuingiza vionjo vya hip hop katika albamu zake, na kufanikiwa kwa wastani. Umaarufu wake aulianza kuisha baada ya kuondoka Columbia mwaka 2001. Baadae alisaini mkataba na studio ya Virgin Records lakini baadae aliachishwa kutoka katika studio hizo, hii ikiwa ni baada ya kupata matatizo ya akili yaliyotangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari, lakini pia ikiwa ni baada ya filamu yake ya Giltter kushindwa kufanya vizuri. Mwaka 2002 Carey alisaini mkataba na studio ya Island Records na baada ya kupata matokeo mabaya katika kipindi cha nyuma, hatimaye alirejea katika chati ya muziki wa pop,. hii ikiwa ni mwaka 2005.[6][7].

Carey ameuza nakala zaidi ya milioni 175, za albamu na single dunia nzima..[8][9][10] Carey alitajwa kuwa mwanamuziki wa kike anayeongoza katika mauzo kwa mwaka 2000, hii ikiwa ni katika tuzo za World Music Awards.[11]. Kwa mujibu wa Recording Industry Association of America, Akiwa ameuza nakala za albamu zaidi ya milioni 62.5, Carey ndiye mwanamuziki wa kike anayeongoza kwa mauzo nchini Marekani na kushika nafasi ya 16 kwa kuuza nakala nyingi zaidi ulimwenguni.[12] . Pia anatajwa kuwa mwanamuziki wa kike anayeongoza katika mauzo nchini Marekani katika wakati wa. Nielsen SoundScan [13]

Pia Carey aliongoza katika single za wanamuziki wanaoimba peke yao nchini Marekani.[14] kwa mwaka 2008. Carey alishika nafasi ya sita katika chati ya Billboard ya "The Billboard Hot 100 Top All-Time Artists", na kumfanya kushika nafasi ya pili kwa wanamuziki wa kike wenye mafanikio zaidi katika historia ya 'Billboard [15] Kama nyongeza katika mafanikio yake katika masoko mbalimbali, Carey pia amefanikiwa kupata tuzo za Grammy zipatazo tano. Pia anajulikana kwa sauti yake yenye uwezo wa kubadilika katika nyakati tofauti.

Maisha na muziki

[hariri | hariri chanzo]

Katika utoto na ujana

[hariri | hariri chanzo]

Carey alizaliwa katika eneo la Huntington, Long Island, katika jiji la New York. Ni mtoto wa tatu na wa mwisho katika familia ya Patricia Carey (née Hickey), ambaye pia likuwa mwanamuziki na Alfred Roy Carey, ambaye ni mhandisi.[16][17] Mama yake alikuwa mwenye asili ya Ireland na baba yake alikuwa mchanganyiko wa Afro-Venezuelan na Mmarekani mwenye asili ya Afrika; babu yake kwa upande wa baba aliyeitwa, Roberto Nuñez, alibadilisha jina lake na kuwa Carey ili aweze kuishi nchini Venezuela kuliko kuhamia nchini Marekani.[18] Carey alipewa jina lake kutokana na wimbo wa "They Call the Wind Mariah".[19]. Wazazi wa Carey walitalikiana wakati akiwa na umri wa miaka mitatu tu..[20]. Akiwa anaishi katika eneo la Huntington, eneo lenye ubaguzi wa hali juu, wakazi wa eneo hili wamewahi kumpa sumu mbwa wa familia hii, na kuwasha moto katika gari lao.[21] . Baada ya kutalikiana kwa wazazi wake, Carey alipoteza mawasiliano ya karibu na baba yake, wakati huohuo mama yake alikuwa akifanya kazi katika sehemu zaidi ya moja ali aweze kutunza watoto wake. Carey alikuwa akikaa katika chumba chake na kufungulia sauti kubwa ya muziki. Carey alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 3, wakati alipokuwa akimwigiza mama yake alipokuwa akifanya mazoezi ya kuimba nyimbo mbalimbali katika lugha ya kilatini..[22]

Carey alihitimu katika shule ya Harborfields High School iliyopo Greenlawn, New York. Akiwa shuleni, amekuwa akishindwa kuhudhuria darasani mara kadhaa kutokana na kuwa mwimbaji katika studio zinazotengeneza muziki wa demo. hii ikapelekea wanafunzi wenzake kumtungia jina la utani la Mirage [23] Carey aliganikiwa kufanya kazi katika kisiwa cha Long,mbapo Kufanya kazi katika kisiwa cha Long, kulimpa Carey nafasi za kufanya kazi na wanamuziki maarufu kama vile Gavin Christopher na Ben Margulies, ambao akiwa nao aliweza kushiriki katika kuandika nyimbo mbalimbali. Baadae alirejea tena katika jiji la New York, ambapo Carey aliweza kufanya kazi na kulipa kodi ya nyumba ikiwa ni pamoja kufanya kazi katika duka la urembo.[24] Hatimaye aliweza kuimba kama mwimbaji wa nyuma katika single ya Puerto Rico ulioimbwa na Brenda K. Starr.

Mwaka 1988, Carey alikutana na Tommy Mottolla wa studio za Columbia Records katika sherehe,ambapo Starr alimpa tepu ya Carey. Mottola baada ya kucheza tepu hiyo, aliipenda. Baadae alimtafuta Carey lakini hakumpata kwani alikuwa ameshalipa. Lakini Mottola alimtafuta Carey na kusaini nae mkataba wa kutengeneza nyimbo na studio hizo. Na huu ndio ukawa mwanzo wa Carey kuingia katika ulimwengu wa muziki.[25]

Mafanikio ya mapema zaidi: 1989–1992

[hariri | hariri chanzo]

Carey alishiriki katika kuandika nyimbo katika albamu yake ya mwaka 1990 iliyofanya vizuri iliyoitwa Mariah Carey, na emeendela kundika nyimbo nyingi kati ya nyimbo zake mwenyewe. Wakati wa kurekodi, Carey ilionesha kutokuridhishwa na utendaji kazi wa waanadaji wake kama vile Ric Wake na Rhett Lawrence, ambao studio za Columbia ziliwaweka ili waweze kufanya albamu yake kuwa ya kibiashara zaidi .[26]. Baada ya matangazo ya muda mrefu,. hatimaye albamu hii ilifanikiwa kufika katika nafasi ya kwanza katika chati ya albamu mia mbili bora ya Marekani Billboard 200 ambapo ilifanikiwa kukaa katika nafasi hiyo kwa wiki kadhaa.Pia iliweza kufikisha single nne, kutoka katika albamu hii katika nafasi ya kwanza, na kumfanya Carey kuwa maarufu nchini Marekani. Lakini ulipata mafanikio kidogo katika nchi nyingine. Shutuma mbalimbali zilizuka kufuatia kuchaguliwa kwa albamu ya Carey katika tuzo za Grammy, lakini hatimaye Carey alishinda tuzo za Grammy katika Mwanamuziki bora chipukizi, na single iliyofanya vizuri zaidi ya Vision of Love[27]Best Female Pop Vocal Performance.[28]

Mafanikio ya kimataifa: 1993–1996

[hariri | hariri chanzo]

Carey na Tommy Mottola walianza mahusiano ya kimapenzi wakati wa kutengeneza albamu yake ya mwaka. 1993. Kenneth Edmonds alishiriki katika kutengeneza albamu hii ambayo baada ya kutoka ndiyo iliyokuwa albamu kutoka kwa Carey yenye mafanikio zaidi ulimwenguni. Albamu hii imekuwa katika chati ya Billboard 200 kwa wiki kadhaa. .[29] It yielded her first UK Singles Chart number-one,[30]

Baadae mwaka 1994, baada ya kutoa wimbo akishirikiana na Luther Vandross wimbo ulioimbwa na Lionel Richie na Diana Rose ulijulikana kama ‘’Endless Love’’ , Carey alitoa wimbo albamu ya ‘’Merry Christmas, Albamu hiyo ilijumuisha nyimbo za kurudiwa kutoka kwa wanamuziki wengine, na albamu hii ilikuwa moja kati ya albamu yake iliyofanya vizuri zaidi nchini Japan [31] Katika miaka iliyofuata, Carey aliibuka kama mwanamuziki mwenye mafanikio zaidi nchini Marekani hususani katika redio za nchi hiyo. .[32]

Sura na mwonekano mpya:1997–2000

[hariri | hariri chanzo]
Carey katika eneo la Edwards Air Force Base wakati wa kutengeneza ideo ya wimbo wa "I Still Believe" mwaka 1998.

Carey na Mottola waliachana rasmi mwaka 1997. Japokuwa mwonekano wa wawili hawa mbele za watu walikuwa wakionekana kuwa na furaha. Lakini Carey alisema kuwa, Mottola alikuwa akimwendesha sana[33]. Walitangaza kuachana kwao mmwaka 1997, na taratibu za talaka zilikamilika mwaka uliofuatia.Muda mfupi tu baada ya kuachana Carey aliajiri mtayarishaji mwingine wa muziki.

Albamu ya Carey iliyofuatia, Butterfly, ilitoka mwaka 1997, na kufika hadi nafasi ya kwanza katika chati mbalimbali. Ikiwa na single kama vile Honey’’ ikimwonesha Carey akiwa katika hali ya kuvutia zaidi kuliko alivokuwa mwanzo. [34]. Anasema kuwa Butterfly imekuwa mwanzo wa yeye kuweza kujiongoza katika muziki.[35][36][37] Mwezi Januari mwaka 2010, Carey alitangaza jina la mvinyo wake utakaokuwa unaitwa Angel Champagne.[38]

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]

Albamu za Studio

[hariri | hariri chanzo]

Albamu za mjumuisho

[hariri | hariri chanzo]

Movies
Mwaka Filamu Kazi Tuzo
1999 The Bachelor Ilana
2001 Glitter Billie Frank Golden Raspberry Award for Worst Actress
2002 WiseGirls Raychel
2003 Death of a Dynasty Herself
2005 State Property 2 Dame's Wifey
2008 You Don't Mess with the Zohan Herself
2009 Tennessee Krystal
Precious Mrs. Weiss Breakthrough Performance Award at the Palm Springs International Film Festival[39][40]
Nominated — Black Reel Award for Best Supporting Actress & Best Ensemble.
Nominated — NAACP Image Award for Outstanding Supporting Actress in a Motion Picture
Nominated — Screen Actors Guild Award for Outstanding Cast in a Motion Picture.
Television
Year Title Role Notes
2002 Ally McBeal Candy Cushnip Episode "Playing with Matches"
2003 The Proud Family Herself Voice
  1. "Recent Births Are Announced", April 10, 1969, p. 2-3. Retrieved on 2022-03-27. Archived from the original on 2021-03-03. "Recent births at Huntington Hospital have been announced as follows ….. March 27 Mariah, Mr. and Mrs. Alfred Carey, Huntington" 
  2. http://www.myspace.com/mariahcarey
  3. Ankeny, Jason. "allmusic ((( Mariah Carey > Overview )))". Allmusic. Macrovision Corporation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2002-11-19. Iliwekwa mnamo 2009-10-22. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  4. "Vision of Loneliness Ilihifadhiwa 5 Septemba 2014 kwenye Wayback Machine." Entertainment Weekly. 25 Septemba 2008
  5. Shapiro, Marc. Mariah Carey (2001). pg. 145. UK: ECW Press, Canada. ISBN 1-55022-444-1.
  6. Lamb, Bill. "Mariah Carey- Comeback of the Year" Ilihifadhiwa 15 Desemba 2007 kwenye Wayback Machine.. About.com. 4 Juni 2005. Retrieved 12 Machi 2008.
  7. Anderman, Joan. "Cary's On". The Boston Globe. 5 Februari 2006. Retrieved 12 Machi 2008.
  8. "Mariah's New Single Available At iTunes on Sept. 15th!". Island Def Jam Music Group. Iliwekwa mnamo 2008-10-13.
  9. "MARIAH CAREY's NEW SINGLE "I WANT TO KNOW WHAT LOVE IS" IMPACTS AT RADIO ON SEPT. 14th". Universal Music Group. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-17. Iliwekwa mnamo 2009-11-14.
  10. "CELEBRATE NEW YEAR'S EVE WITH MARIAH CAREY!". Mariah Carey official website. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-11-09. Iliwekwa mnamo 2009-11-14.
  11. "Winners of the World Music Awards". World Music Awards. Mei 2000. Retrieved 19 Novemba 2006 from the Wayback Machine; "Michael Jackson And Mariah Carey Named Best-Selling Artists Of Millennium At World Music Awards In Monaco" Ilihifadhiwa 17 Juni 2010 kwenye Wayback Machine.. Jet. 29 Mei 2000. Retrieved 19 Novemba 2006.
  12. "Gold and Platinum - Top Selling Artists" Ilihifadhiwa 1 Julai 2007 kwenye Wayback Machine.. Recording Industry Association of America
  13. "BLABBERMOUTH.NET - METALLICA Among Top-Selling Artists Of SOUNDSCAN Era". Roadrunnerrecords.com. Iliwekwa mnamo 2009-10-21.
  14. Pietroluongo, Silvio. Mariah, Madonna Make Billboard Chart History Ilihifadhiwa 23 Oktoba 2008 kwenye Wayback Machine.. Billboard. 2 Aprili 2008. Retrieved 2 Aprili 2008.
  15. "Billboard Hot 100 Chart 50th Anniversary", Billboard. Retrieved on 2009-10-01. Archived from the original on 2008-09-13. 
  16. Shapiro, pg. 16.
  17. "Mulatto - An Invisible American Identity" Ilihifadhiwa 10 Machi 2009 kwenye Wayback Machine.. racerelations.about.com. Retrieved 3 Aprili 2008.
  18. "Alfred Roy Carey". Mariahcareyfanclub.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-09-25. Iliwekwa mnamo 2009-09-11. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help)
  19. People.com: Mariah Carey. People. Retrieved 3 Aprili 2009.
  20. Shapiro, pg. 19-20.
  21. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named smellperfume
  22. Shapiro, pg. 18–19.
  23. Shapiro, pg. 31.
  24. Handelman, David. "Miss Mariah." Cosmopolitan. Desemba 1997.
  25. Gardner, Elysa. "Cinderella Story." VIBE. Aprili 1996.
  26. Shapiro, pg. 47, 60.
  27. "Mariah Carey > Charts & Awards (Grammy Awards)". AllMusic.com. Iliwekwa mnamo 2008-07-05.
  28. Ankeny, Jason (2008-04-15). "Mariah Carey > Biography". AllMusic.com. Iliwekwa mnamo 2008-07-05.
  29. "Music Box - Mariah Carey". Billboard. 6 Oktoba 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-03. Iliwekwa mnamo 2010-01-24. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)
  30. "The UK Number Ones: Double Tops". A Half Century of British Number Ones. Retrieved 2 Januari 2008.
  31. "Single Sales Ranking (Mariah Carey)" (kwa Japanese). oricon. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-25. Iliwekwa mnamo 2008-11-02.{{cite web}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
  32. "Mariah Carey – Billboard Singles". Allmusic. Retrieved 19 Septemba 2006.
  33. Shapiro, pg. 97–98.
  34. Shapiro, pg. 101; Handelman.
  35. "Sonia, Tata in Time's most influential list" Ilihifadhiwa 5 Mei 2009 kwenye Wayback Machine.. expressindia.com. 1 Mei 2008. Retrieved 1 Mei 2008.
  36. "Tony Blair makes list of 100 most influential people – but there's no place for Gordon Brown". Daily Mail. 1 Mei 2008. Retrieved 1 Mei 2008.
  37. "Mariah Carey" Ilihifadhiwa 4 Mei 2009 kwenye Wayback Machine.. Time. 1 Mei 2008. Retrieved 1 Mei 2008.
  38. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named Carey
  39. "Morning Roundup: Mariah Carey Wins Acting Award". The Wall Street Journal. 24 Novemba 2009. Retrieved 25 Novemba 2009.
  40. "Mariah Carey" Ilihifadhiwa 4 Mei 2009 kwenye Wayback Machine.. Variety. 23 Novemba 2009. Retrieved 25 Novemba 2009.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: