Boyz II Men

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Boyz II Men
Boyz II Men performing at Vega, Copenhagen.
Taarifa za awali
Miaka ya kazi1985–hadi sasa
StudioMotown, Universal Music Group, Universal, Arista Records, Arista, MSM, Koch, Decca, UMG
Ameshirikiana naL.A. Reid, Babyface, Mariah Carey, Tim & Bob, Jimmy Jam and Terry Lewis, Sean Combs, Dallas Austin, Brandy, Uncle Sam, New Edition, 112, Brian McKnight, Vivian Green, Bell Biv DeVoe
Wavutiboyziimen.com
Wanachama

Boyz II Men ni kundi la muziki wa R&B kutoka mjini Philadelphia, Pennsylvania, Marekani. Wanafahamika zaidi kwa ukali wao wa kuimba sauti tupu na hamoni. Kwa sasa wapo watatu tu, Nathan Morris, Wanya Morris na Shawn Stockman. Wakati wa miaka ya 1990, Boyz II Men waliupatia umaarufu wao kupitia studio ya Motown Records wakiwa wanne na Michael McCary, ambaye ameondoka kundini mnamo mwaka 2003 kwa kufuatia masuala mbalimbali ya kiafya.[1]

Katika miaka ya 1990, Boyz II Men walipata umaarufu na mafanikio makubwa sana si ndani tu bali hata kimataifa. Hii ilianza kwa kutoa kibao cha "End of the Road" mnamo 1992, ambacho kilibamba chati mbalimbali duniani.[2] "End of the Road" ilileta rekodi mpya kwa kukaa muda mrefu kwenye chati, kilishika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot 100 kwa majuma 13, ilivunja rekodi iliyowekwa miongo kadhaa nyuma na marehemu Elvis Presley. Boyz II Men waliendelea kuvunja rekodi kwa kutoa kibao cha "I'll Make Love to You" na "One Sweet Day" (wameimba na Mariah Carey), ambacho kilikaa kwa majuma 16 mfululizo, vyote vilivunja rekodi kwa kukaa nafasi ya kwanza. Haikushia hapo, "I'll Make Love to You" imevuka mipaka na kushika nafasi za juu kabisa huko nchini Australia (kwa kushika nafasi ya kwanza kwa majuma manne) na kupata mafanikio mazuri kimataifa. Mpaka 2017, "One Sweet Day" bado inashikilia rekodi yake ya kukaa majuma 16 kwenye chati za Hot 100, kiasi imejitahidi Despacito.

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Studio albamu


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Boyz II Men Dishes On Mike, Their Estranged Fourth Member". Huffington Post. Iliwekwa mnamo 2014-10-30.
  2. Billboard. [Boyz II Men katika Allmusic "(Boyz II Men > Charts & Awards > Billboard Singles)"]. AllMusic. Iliwekwa mnamo 2010-05-16. {{cite web}}: Check |url= value (help)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: