Mataifa ya Kati
Mataifa ya Kati yalikuwa ushirikiano wa nchi zilizoshikamana katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia dhidi ya Mataifa ya Ushirikiano. Nchi hizo zilikuwa Ujerumani, Austria-Hungaria, Milki ya Osmani (baadaye Uturuki) na Bulgaria.
Nchi hizo zilipigana na Ufaransa, Uingereza, Ubelgiji, Ureno, Serbia, Urusi na Italia. Tangu mwaka 1917 Urusi ilitoka katika vita lakini Marekani na nchi mbalimbali zilingia upande wa ushirikiano, mfano Najd (baadaye Saudia), Japani, na nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini.
Mataifa ya Kati yalishindwa; tokeo la vita lilikuwa mwisho na mgawanyo wa Milki ya Osmani na Milki ya Austria-Hungaria, pamoja na kutokea kwa idadi ya nchi mpya katika Ulaya ya Mashariki (Poland, Chekoslovakia, Kroatia), na kukabidhiwa kwa makoloni ya Ujerumani (Namibia, Togo na Kamerun pamoja na Tanganyika, Rwanda, Burundi) kwa nchi nyingine kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mataifa ya Kati kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |