Nenda kwa yaliyomo

Wafiadini wa Mombasa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mashahidi wa Mombasa)

Wafiadini wa Mombasa ni kundi la Wakristo Wakatoliki zaidi ya 280 waliouawa na sultani Jeromino au Yusufu Chingulia huko Mombasa (leo nchini Kenya) tarehe 21 Agosti 1631 kwa sababu ya imani yao, ambayo mwenyewe alikuwa ameikana ili kurudia Uislamu.

Kati yao kuna Wareno wengi (wanaume 47, wanawake 39 na watoto 59), lakini Waafrika labda wengi zaidi (wanaume 72, mbali ya wanawake na watoto) waliomuamini Yesu kwa dhati wasiweze kumkana kwa lolote.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 16 Agosti 1631, sultani huyo alikusanya watu kutoka bara akavamia Fort Jesus kwa kujifanya anataka kushiriki ibada. Kumbe alimuua kapteni Mreno kwa kisu, wakati wafuasi wake walipochoma moto mji mzima.

Wakazi walikimbilia nyumba ya wamisionari Waaugustino. Hapo suala halikuwa tena kufukuza Wareno tu, bali kukomesha Ukristo.

Sultani aliwatolea wote nafasi ya kusilimu ili kukwepa kifodini, lakini mmoja tu alikubali. Watu wake walishambulia kanisa tarehe 20 Agosti huku wakiua wote waliolikimbilia.

Kesho yake wanawake wengine pamoja na watoto, wakiwemo Wareno na Waafrika, walipita kati ya mji wakiimba tenzi za Kikristo. Walilazimishwa kupanda boti walioangamizwa kwa visu na mikuki.

Isabel Varella alikataa kuasi, lakini alifanywa mtumwa badala ya kuuawa. Hata mke na binti walifia dini yao.

Sultani Yusufu (Jeronimo) aliondoka Mombasa mwaka 1632 akawa haramia kwenye Bahari ya Shamu.

Siku hizi kesi ya kuwatangaza hao wafiadini kuwa wenye heri na halafu watakatifu inaendelea.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wafiadini wa Mombasa kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.