Maria Nyerere
Maria Nyerere | |
Maria (kulia) na Evelyn Macleod | |
Mke wa rais wa kwanza wa Tanzania
| |
Muda wa Utawala 29 Oktoba 1964 – 5 Novemba 1985 | |
mtangulizi | Mwanzilishi |
---|---|
aliyemfuata | Siti Mwinyi |
Mke wa rais wa Tanganyika
| |
Muda wa Utawala 9 Disemba 1962 – 25 Aprili 1964 | |
tarehe ya kuzaliwa | 31 Desemba 1930 Tanganyika |
utaifa | Mtanzania |
chama | Chama Cha Mapinduzi |
ndoa | Julius Nyerere (1953-1999) |
watoto | 7
|
mhitimu wa | Sumve Teacher Training College |
Fani yake | Mwalimu |
dini | Mkristo - Katoliki |
Maria Nyerere (alizaliwa kama Maria Waningu Gabriel Magige[1] mnamo 31 Disemba 1930[2][3]) alikuwa mke wa rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Kambarage Nyerere kuanzia 1964 hadi 1985.[4] Kwa kawaida nchini Tanzania anajulikana kama 'Mama Maria' tu.[5][6]
Alikuwa mtoto wa saba kati ya tisa wa Gabriel Magige, wa Baraki, Tareme[7], kutoka kwa mkewe Hannah Nyashiboha.[8]
Maria alisoma katika shule "White Sisters' School" iliyokuwa Nyegina, kisha shule ya Ukerewe, kisha akajiunga na chuo cha ualimu "Sumve Teacher Training College"; alihitimu kwa kupata cheti cha ualimu akaanza kufundisha katika Shule ya Msingi Nyegina iliyoko Musoma.[9] Aliolewa na Julius Nyerere mwaka 1953.
Kwa sasa ni miongoni mwa wajumbe saba wa baraza la wazee wa "Alliance for Tanzania Youth Economic Empowerment" (Atyee), pamoja na rais wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi na rais wa zamani wa Zanzibar Amani Abeid Karume ambaye alikuwa mtoto wa Rais wa kwanza wa Zanzibar.[10]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Nyerere and Africa: End of an Era, Godfrey Mwakikagile, New Africa Press, 2007, pg 403
- ↑ https://mobile.twitter.com/tanzaniahistory/status/815211458787209216
- ↑ Nyerere: The Early Years, Thomas Molony, 2014, pg 89
- ↑ "Profile: Nyerere". juliusnyerere.info. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Julai 2013. Iliwekwa mnamo 23 Mei 2013.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ http://www.monitor.co.ug/Magazines/Full-Woman/Mama-Maria--Keeping-Mwalimu-Julius-Nyerere-s-candle-alight/-/689842/2346950/-/38nwks/-/index.html
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-22. Iliwekwa mnamo 2018-05-19.
- ↑ Nyerere and Africa: End of an Era, Godfrey Mwakikagile, New Africa Press, 2007, pg 628
- ↑ Nyerere: The Early Years, Thomas Molony, 2014, pg 89
- ↑ Nyerere: The Early Years, Thomas Molony, 2014, pg 90
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-21. Iliwekwa mnamo 2018-05-19.
Makala hii kuhusu wasifu wa Mtanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |