Nenda kwa yaliyomo

Ugonjwa wa kuambukiza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Maradhi ya kuambukiza)
Bakteria ya "streptococcus pneumoniae" ni pathojeni inayosababisha kifua kikuu.
Wadudu kama mbu huyu wanaweza kupeleka pathojeni kutoka mgonjwa mmoja hadi mwingine.
Kunawa mikono ni njia rahisi ya kuepukana na maambukizo mengi.

Ugonjwa wa kuambukiza (kwa Kiingereza infectious disease) ni ugonjwa wowote unaosababishwa na ambukizo, yaani kuingia na kuenea kwa pathojeni kama bakteria, virusi au fungi katika mwili. Wanadamu, wanyama na pia mimea wanaweza kuambukizwa na pathojeni hizi.

Njia za maambukizo

[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya magonjwa hayo yanaweza kupitishwa na mgonjwa mmoja kwenda kiumbehai mwingine. Njia za kuambukizwa (yaani njia ya kufika kwa pathojeni mwilini) ni nyingi, zikiwa pamoja na kugusana, maji, chakula, damu au hata hewani.

Pathojeni kama visababishi

[hariri | hariri chanzo]

Pathojeni ni jina kwa bakteria, virusi au fungi zinazoweza kusababisha ugonjwa. Si kila bakteria au fungi inasababisha ugonjwa, kinyume chake tunaishi kwa kuwa na mamilioni ya bakteria katika utumbo ambazo ni lazima kuwepo kwa afya yetu. Vidubini hivyo vyote ni vidogo mno, havionekani kwa macho.

Dalili za magonjwa

[hariri | hariri chanzo]

Magonjwa ya kuambukizwa huwa na dalili tofauti sana. Mara nyingi dalili za ugonjwa hutegemeana na pathojeni iliyosababisha ugonjwa. Dalili zinaweza kuonekana siku chache baada ya kuambukizwa au kuendelea kusambaa polepole katika kipindi cha wiki, miezi hata miaka.

Kingamwili na maambukizo

[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida mgonjwa anapona mwenyewe na mfumo wa kinga mwilini unajifunza kupambana na pathojeni husika. Kama inarudi mwili unaijua tayari, hivyo si kawaida mtu kugonjeka mara mbili na ambukizo lilelile.

Kwa mtu mwenye kingamwili nzuri maambukizo yanaweza kupita kwa kuonyesha dalili chache tu au hata bila dalili yoyote. Kwa watu wengine dalili za ugonjwa zinaweza kuwa nzito mno na kuhatarisha maisha.

Suala muhimu ni uwezo wa mfumo wa kinga kutambua na kuondoa kisababaishi cha ugonjwa yaani pathojeni. Leo hii sayansi ya tiba imekuta madawa dhidi ya pathojeni kama vile antibiotika dhidi ya bakteria, antimykotika dhidi ya fungi na virostatika dhidi ya virusi.

Kuna pia uwezekano wa kupiga chanjo dhidi ya virusi kadhaa. Lakini magonjwa ya kuambukizwa mengine hayana tiba hadi leo na magonjwa mapya yanaweza kutokea.

Makadirio ya vifo duniani kutokana na magonjwa ya kuambukiza kadiri ya WHO

[hariri | hariri chanzo]
Ugonjwa wa kuambukizwa Idadi ya vifo kwa mwaka
Magonjwa ya njia za pumzi milioni 3.9
UKIMWI milioni 2.8
Magonjwa ya kuhara milioni 1,8
Kifua kikuu milioni 1,6
Malaria milioni 1,3
Surua (morbilli) 611.000
Kifaduro 294.000
Pepopunda (tetanus) 214.000
Meningitis 173.000
Kaswende (syphilis) 157.000
Homanyongo (hepatitis B) 103.000
Malale 48.000
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ugonjwa wa kuambukiza kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.